
Ulinzi ni mkali kweli kweli zaidi na polisi 10,000 wamemwagwa jiji la Nairobi kwa ajili yakulinda usalama kwa ujio wa Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama anayetarajiwa kuwasili jijini Nairobi siku ya Ijumaa kati ya saa 1;45 na 2;35 jioni ya siku hiyo ya July 24, 2015.
Baadhi ya barabara za jiji la Nairobi zimefungwa kwa ajili ya kuimarisha usalama wa jiji hilo wakati wa ujio wa Rais huyo wa Marekani.
Anga la nchi hiyo litafungwa siku ya Ijumaa mida hiyo ya Rais Obama atakapo wasili ni siku ya Jumapili jioni Rais Obama atakapoondoka nchini humo..Shirika la Anga nchini Kenya KCAA limetangaza siku ya Ijumaa kati 1;45 na 8;35 hakutaruhusiwa kwa ndege yeyote kuruka au kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo kenyata na hivyo hivyo ndivyo itakavyokua siku ya Jumapili kati ya 11;05 na 11;45 jioni Rais Obama atakapokua amemaliza ziara nchini humo/
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake