Thursday, August 20, 2015

HII ILIANDIKWA MWAKA 2011 KUHUSU UHUSIANO WA LOWASSA NA FREEMAN MBOWE NA MAZUNGUMUZO YAO YA SIRI YALIVYONASWA

Na Mwandishi wetu, Gazeti la Sauti Huru

Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.

Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)

Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.

Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"

Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.

" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;

"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".

...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'

"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.

Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "

"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"

Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.

"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"

"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."

6 comments:

  1. Mtapanda na kupandikiza CCM
    Mbona udhaifu wa Magufuli na CCM yenu hamvisemi

    ReplyDelete
  2. Pole Lowassa
    CCM wanakutafuta kila kona
    Picha ile ile wanabadilisha vinywa vya habaril
    Na sisi tuliopo ughaibuni ukiona mtu anaisifia CCM ana maslahi yake

    Halipi kodi akipeleka biashara bongo
    Mwacheni lowassa tutkutane 25 October

    ReplyDelete
  3. TUACHENI KUYUMBISHA WATANZANIA PICHA HII HII ILITOLEWA TENA MAJUZI WAKATI WA MADAI KUWA ANAJIUNGA CDM. Unajua tatizo moja waandishi nao wananjia mojawapo ya kununuliwa hivyo hatuoni haja ya kutuletea gumzo lile lile. tusubirie ufike wakati muafaka.

    ReplyDelete
  4. Afadhali wadau mmeliona hilo mnaakili sana siyo Yale majinga yenye upungufu Wa kufikiri yangeanza kutetea ccm hapa wachangiaji wote wangekuwa na akili kama nyinyi am sure taifa letu litabadilika na kutoka kwa hawa mabepari Wa ccm

    ReplyDelete
  5. Kama haya yote tunayoyasoma na tunayoyasikia yana ukweli ndani yake basi nchi iko katika hali ngumu na Watanzania kwa ujumla wetu inabidi tuamke na kuwa macho sana hususan wakati huu tunapoelekea katika upigaji kura wa kuchagua kiongozi wetu ajae. Kama pesa zinatumika kununua nafasi za uongozi au kuhamasisha idadi kubwa ya wananchi kujiunga kwenye misafara ya viongozi, hili ni kosa kubwa na linapingana na maadili ya sheria za uchaguzi. Pamoja na haya yote, muda wa kampeni haujaanza lakini tunashuhudia misafara mirefu ya viongozi ikiendelea kutembelea sehemu mbalimbali ya nchi ikijinadi kinyume na maagizo ya Tume ya Uchaguzi. Makosa kama haya mara nyingi yamekuwa ndio sababu kubwa ya kupelekana mahakamani. Tayari kuna wengine wameshatishia hata kuruka mahakama zetu nchini na kwenda moja kwa moja kwenye Mahakama ya Kimataifa (ICC). Mfano hapa ni tuhuma na vitisho vilivyotolewa kwa vyombo vyetu vya Usalama ambavyo vishutumiwa kuwa vinatumika na baadhi ya vyama. Bila kuwa na ushahidi au maelezo ya kina vyombo hivi vinatumikaje tunaweza kuelezea kuwa huu ni uchochezi tu ambao hauna faida yoyote kwa Watanzania wengi tupendao amani.
    Mimi ni Mtanzania niliyeko huku Ughaibuni na natoa mchanganuo wangu huu kuonyesha upendo wangu kwa nchi yangu, na upendo huu hauna masharti wala mfungamano wa kichama. Maslahi yangu ni kuwa Mtanzania na hakuna zaidi ya hapo.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake