ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 10, 2015

KAZI ZASIMAMA JIJINI DAR KUPISHA LOWASSA ACHUKUE FOMU YA KUWANIA URAIS

MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa amechukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kuwania nafasi hiyo leo Jumatatu Agosti 10, 2015.

Msafara wa Mgombea huyo ulioanzia kwenye Ofisi za Chama cha Wananchi CUF Buguruni na kuishia kwenye Ofisi za CHADEMA Kinondoni Jijini Dar es salaam na kupelekea msongamano mkubwa wa watu ambao wengi wao ni wafuasi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA, na kufanya shughuli mbali mbali kusimama kwa muda wa takribani saa saba.  
Umati wa watu wakiwemo wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA ukiwa Umefurika kwa wingi kwenye Barabara ya Uhuru, Jijini Dar es salaam kumsindikiza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapingua maelfu ya wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA, jijini Dar es salaam, Augusti 10, 2015, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakati alipofika kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za tume ya Taifa ya Uchaguzi kkugombea nafasi hiyo, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhan Kombwey, baada ya kukabidhiwa fomu za tume hiyo za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Agosti 10, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif.
Mh. Lowassa na Mh. Duni wakiwapungia maelfu ya wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA nje ya Makao Makuu ya Chama cha CUF, Buguruni jijini Dar.

Sehemu ya Wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA wakiushangilia Msafara wa MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa wakati akielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.
Buhuruni Rozana.
MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama cha CUF, Buguruni Jijini Dar es salaam.
MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mh. Freeman Mbowe, huku Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akishuhudia.


Mh. Freeman Mbowe, Mh. Tundu Lissu na Mh. James Mbatia wakiwa kwenye magari yao wakati wakimsindikiza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.
Barabara ya Uhuru, Jijini Dar.
Barabara ya Bibi Titi Mohamed, Jijini Dar.
Barabara ya Uhio.
Hakuna alietaka kupigwa na tukio hili.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapingua maelfu ya wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA, jijini Dar es salaam, Augusti 10, 2015, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.







Mgombea mwenza wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwapungia wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA, jijini Dar es salaam, Augusti 10, 2015, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.













7 comments:

Unknown said...

Picha za kupanga pamoja na kununuwa watu unafikiri zinawashughulisha CCM.Yeye hataalete watu wa kukodi kutoka nchi jirani maana naona hao waliotoka Arusha na moshi hawakutosheleza vizuri basi kwa maghufuli atafulia tu .

Anonymous said...

Hivi watu wengine huwa ni vichaaa au anashilngi ngapi kununua watu wote haoo na haoo walioko kwenye magorofa kanunua pia..

Anonymous said...

Wewe mdau wa kwanza unapointi isio na maana next time jaribu kutofikiria kama jembe na nyundo kwani vimepitwa na wakati, fikiria maendeleo trekta na nail gun

Anonymous said...

Mpuuzi wa juu hapo marlon ndiyo nyimbo zenu sisiemu mara fisadi kumbe maamuzi yametoka kwa mkubwa wake(Richmond)mara ananunua wafuasi hizo dalili za mfa maji mimi sina chama ni mpiga kura lakini sasa nadhani ni wakati wa chama chako kupumzika sasa. na kwa taarifa yako hawa watu wengine ni kutoka chama chako.najua ni ngumu sana kuyaamini mabadiliko ya kihistoria lakini yako njiani mwaka huu. Hata marekani weusi walikuwa hawamuungi mkono Obama lakini aliposhinda jimbo la weupe IOWA hata weusi walijua yes he can.Na huyu jamaa siyo mrema ana system kubwa sana ya ndani na nje ya sisiemu.

Anonymous said...

Jipe moyo anonymous wa kwanza ili uendelee kuishi mpaka October,unafikiri watu wanauza nyago?na kwa taarifa yako waendesha boda boda mpaka mateja wamejiandikisha kupiga kura, hii ni 2015 siyo 1995 ya mrema.

Anonymous said...

Ushabiki tu wa vyama tumekuswanywa kibao kitaaa kumshangilia Raisi wa kanda ya kas kazini, ,, raisi wq tanzania Magufuli tuuuu bora jeshi lichukue nchi kuliko kupewa Lowasa habarI ndio hiyo.

Anonymous said...

wana ccm huko marekani ni aje?mafuriko mnaweza kweli kuyazuiya kwa mikono?
mtashinda kwa goli la mkono?ninavyo hisi mimi.