Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli akikabidhi hati ya Kiapo mapema leo mchana kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Sekieti Kihiyo (katikati). Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli akisaini hati ya Kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Jaji Sekieti Kihiyo mara baada ya kusaini hati ya kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa ndani ya moja ya chumba cha Mahakama Kuu wakirekodi tukio la Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli sambamba na mgombea Mwenza,Samia Suluhu Hassan walipokuwa wakisaini hati ya Kiapo mapema leo mchama Mahakamani Hapo mbele ya Jaji Sekieti Kihiyo.
Mgombea urais wa chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nje ya jengo la Mahakama Kuu mara baada ya kusaini hati ya Kiapo mapema leo mchana.Hati hiyo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. PICHA NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.
Kama kuna losa kubwa lililofanyika kwenye upembuzi pale Dodoma. Basi kubwa ni hilinla mgombea Mwenza. Mhe. Rais anaelewa kabisa alikoipeleka nchi hii hadi anapoondoka madarakani na kwa namna yeyote iwayo hii serikali ijayo inahitaji kiongozi mkali na anayewajibika na kuwajibisha wazembe wala rushwa, kusimamia mapato ya taifa. Watu kifanya kazi ipasavyo sio lelemama zinazoendelea na matokeo yake kuendeleza rushwa. Maeneo.menhi sana ya kutengenezea sehemu za kupumzikia na viwanja zimepewa wenyewe!! Je mhombea mwenza atayaweza.
ReplyDeleteMhe. Magufuli ukifanikiwa kwa kweli una kazi kubwa mbele yako! Je huko hazina umeshauliza kumebakia nini? Au na wewe utakuwa na safari lukuki? Hawa wala rushwa na wagawanaji wa ESCROW utawawezaah?
ReplyDeleteHamna kitu hapa!
ReplyDelete