Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Jangwani.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 -2020
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye uzinduzi wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani.
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakionyesha Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 katikati ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye aliwakabidhi ilani hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM Jangwani.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikweteakizungumza baada ya kukabidhi ilani kwa mgombea wa CCM
Umati wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM Jangwani.
Hii ndio CCM
TOT wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa bongo wakiwa jukwaani.
Hiyo ndio CCM banaaaa Chama kimoja tu nyomi ya watu mtatukana sanaaa,,,,kwenye mablog yenu ila ukweli unabaki palepale Nabari moja ni CCM.
ReplyDeleteNambari 1 CCM nambari 0 ni mwananchi !! Mwenye ubongo na macho haambiwi tazama miaka 50 ilivyo tutia umaskini
ReplyDeleteNyomi nini nansie tumo humo.humo tunawacheki tu
ReplyDeleteccm nyomi nyomi tu
ReplyDeleteccm ndio dawa yao mpaka watanyooka
ReplyDeleteKazi nzuri wamefanya organizers na pia wamechagua siku nzuri. Visual analysis inaonyesha segment ya wapiga kura wenu wengi, wanawake na wazee. Ila ikumbukwe tu kuwa ni juhudi zilofanyika kuchukua watu hadi mikoa ya jirani, watoto wa shule n.k na kubwa zaidi CCM imepatiwa all means necessary na vyombo vya usalama kuhakikisha mkusanyiko unakuwa mkubwa.
ReplyDeleteWell, ombi au angalizo langu ni kuwa, the same level field should be provided to other side. Experience inaonyesha kuwa, gathering ya UKAWA hapo katika eneo hilo itakuwa maradufu zaidi ya hiyo, sasa sitatamani kuona vyombo au authority yoyote ianze kuweka mizengwe au kuchimba mikwala wakati na wao wakifanya maandalizi ya mkutano wao.
Mmekusanyika kwa wingi, mmecheza ngoma, kutoa sera zenu na siku imepita, then please give them also similar opportunities.
Watakuwa wengi for sure, na watafurahi na kutoa sera zao.
Msiogope.
Wewe unaebeza kwamba miaka 50 tangu upatikane uhuru hakuna kilichofanyika na tungali masikini wewe ndo ubongo wako umejaa matope na sitashangaa nikisikia kwamba umehifadhiwa katika jela ya watu wenye matatizo ya akili ambao wapo hatari kuhatarisha maisha ya wengine. America, USA 140years baada ya uhuru wanaake hawakuwa na haki sawa na wanaume kwa namna yeyote ile unaoifahamu wewe. 100years America( usa)baada ya kujipatia uhuru wake toka uengereza watu weusi walibakia kuwa watumwa na kufanyishwa kazi bure, mtoto akizaliwa na familia ya kitumwa hawana haki ya Yule mtoto waliemzaa bali ni wa tajiri anaewamiliki na mmiliki huyo wa watumwa anauwezo wa kumchukuwa huyo mtoto na kumuuza kwa tajiri mwengine bila ridhaa ya wazee wake . Moja ya vitu vilivyokuwa vinawasonenesha familia za kitumwa ni jinsi familia zao zilivyokuwa zikitengenishwa bila ya matakwa yao. Baba anatengenishwa na mke na watoto kwa kuwa tu kaja tajiri mwengine na angependa kuwa na Yule mtunwa mwanamme peke yake na angetoa dau zuri kidogo kumbuka mtumwa hapa anauzwa kama ng'ombe hakuna chore chore yeye anachonufaika na mauzo sana machugu ya kuicha familia yake. Takribani miaka mia mbili 200 Wamerikani wamehangaika kujinasua katika hali ya kiuchumi , kisiasa na kiusawa wa haki za watu wote. Hizo za haki sawa kwa wote sisi tunaoishi ndani humu hasa tunaoishi kwenye hood ndio tunaojua hali iko vipi . Kwa hivyo huo ni muhtasari tu ya kwamba haifai kabisa kubeza yaliyofanyika ndani ya miaka 50 tangu uhuru kama wewe kweli ni mtanzania sio mkanzania. Labda iwe wewe mwenyewe hujitambui au kuna watu wanajiita mahidhibu hasa kule Zanzibar wao wameapa hakuna kizuri kitachofanyika Tanzania na Zanzibar kwa ujumla wakakiunga mkono kwa madai ya kwamba utawala wa mtu mweusi haukuwa wa haki sasa wanatumia huu mwanya wa vyama vingi labda wanaweza kusimamisha serikali wanaoitaka wao lakini hicho sio kitu rahisi kwa watanzania wa leo na dunia kwa ujumla.
ReplyDeleteMakada wa ccm hasa wale wenye uelewa duni wanaendelea kupiga porojo juu ya Afya ya Mh Edward Lowasa, ni haki yao kutoa maoni ili taifa lipate rais bosa na mwenye afya bora.
ReplyDeleteLakini kinachoshangaza nikuona watu hawa wanajipa jukumu la utabibu na kusimulia kile wakiitacho “ugonjwa” wa Lowasa,
Ukiwauliza Lowasa anaumwa nini? Hakika watakupa kila mtu jibu lake na ukimrudia tena mmoja mmoja kumuuliza atakwambia jibu tofauti na la awali, mara oooho Lowasa ana kisukari, mara ana kiharusi, mara ana kisend off nk, ilimradi tu waonekane wamesema.
Ukiwauliza tena vipi afya ya Magufuli? Majibu yao ni kama wapo ahera vile,
Hizi ndio siasa za kiswahili na waswahili wenyewe ndio sisi. Watanzania wengi huenda hawafahamu hili,
Dr John Pombe Magufuli ni mgonjwa wa Moyo tangu mwaka 2000, na mwaka 2014 alikwenda kufanyiwa upasuaji mkubwa nchini ujerumani mjini Born, hivi hapo alipo Magufuli anatumia moyo wa bandia, na ikitokea mjanja yoyote yule aka hark software ya hospitali ile pale borne basi Magufuli ata stuck na kufa,
Kila mwaka anatakiwa aende kuuchaji ambapo mwaka huu atakwenda 26/12/2015.
Hilo wanaccm kindakindaki hawalifahamu, lakini Jakaya,Othuman, Mkapa, Pia Lowasa, Mbowe, na Madaktari bingwa wa moyo pale MOI wanajua vema.
Masuala ya afya yakihojiwa sana kishabiki watu wawe tayari kupokea ukweli uliojificha!
Mimi sijui ugonjwa wa Lowasa wala yeye hajui ugonjwa wangu bali madaktari wetu ndio hujua. Lowasa ni mzima, hakuna hospitali nchini na dunia iliyotoa taarifa za ugonjwa wake na kuwa hastahili kuwa Rais wa Tanzania.”