Jiji la Dar es Salaam limepiga marufu maandamno yeyote ya vyama vya siasa hasa wakati wa kampeni na kwamba kufanya hivyo ni kinyume na sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa chama au wafuasi wowote watakaobainika kufanya maandamo hayo.
Agizo hilo
kali kwa wafuasi na vyama vya siasa imekuja siku moja tu kabla ya kuanza
kampeni za uchaguzi mkuu, ambapo kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
vyama vyote vya siasa na wafuasi wao watakaofanya kampeni zao Dar es Salaam
hawanabudi kuachana na dhana ya maandamo kuelekea kwenye viwanja vya mikutano
kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Kwa upande
wa jeshi la polisi wanasema wako imara katika kutekeleza agizo hilo na kwamba
hawatovumilia chama au kikundi chochote kitakacho sababisha uvunjaji wa amani
katika kipindi cha kampeni.
Katika
hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka watendaji katika mitaa
kutokukubali watu watakaokufa kwa kipindupindu kuzikwa na ndugu zao kwani
inaweza kuwa chanzo cha kuzidi kusambaza ugonjwa huo.
Kwa mujibu
wa maafisa wa afya wanasema ugonjwa huu wa kipindupindu wakati wa kiangaza
husambaa haraka zaidi, huku ulaji vyakula vilivyopoa, kutokunawa mikono vizuri,
ulaji hovyo wa matunda vikitajwa kuwa moja ya sababu za ugonjwa huo.
Kwa mujibu
wa taarifa hiyo aliyoitoa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mpaka
sasa kunawagonjwa 36 wa kipindupindu huku wagonjwa wapya wakiwa 9 ambapo kata
zilizo athirika zaidi zikiwa ni Mwananyamala, Manzese, Saranga, Kimara,
Ubungo,Kigogo, Tandale na Kijitonyamalas.
Chanzo: ITV Tanzania
Chanzo: ITV Tanzania
2 comments:
NINI MAANA YA UHURU? SAME TACTICS ZILIKUWA ZINATUMIWA NA WAKOLONI KUWANYAMAZISHA WANANCHI.
Mtatumia mbinu za aina zote, lakini sisi na Lowassa. Tunataka mabadiliko. Mbona ccm wamefanya sana mikutano yao kwa maandamano, hamjayazuia. Au mmeona haya mafuriko mtashindwa kuyazuia mnanona ni vema mkaanza kuweka vizingiti vya aina hii. Said, kikwete, na kina nape na kinana angalieni jamani, hii nchi siiiii yenu...mmpewa dhamana tu, kesho mtakaa pembeni, na tukishakuchukua nchi sisi waTeamLowassa hatutafanya vitu vya kidikteta ndani ya nchi namna mnavyofanya. Huu ni udikiteta, si demokrasi. Polisi wanatakiwa tu kuelezwa kwamba kutakuwa na maandamano ya kwenda kwenye viwanja vya mkutano. Wao wanalipwa na kodi zetu kutoa ulinzi! Lakini hata uwanja wa Taifa mnaugomea? Iweje? Mungu mmbariki Raisi wetu wa awamu ya nne na ya ya Tano, Edward Lowassa. Nasema, na ninarudia, Edward Lowassa ni raisi wa awamu ya nne na ya tano - kwa sababu inabidi asafishe kila kitu kichafu kilifonywa na huyu bwana. Nyumba (Tanzania) inanuka rushwa nyufa zinaota kila mahali
Post a Comment