Watu tisa waliokuwa wakisafiri na
gari dogo aina ya noah namba T812 BJU, wamefariki dunia papo hapo
baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka jana jioni.
Ajali hiyo imetokea saa 11 jioni
katika kijiji cha Mwamanga wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza kwenye
barabara kuu ya kutoka Shinyanga kuelekea Mwanza, wakati gari hilo
kumshinda dereva wake ambaye ni koplo mstaafu wa jeshi, Moris
Lukenza, mkazi wa Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo, kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Charles Mkumbo, amesema gari
hiyo imepata ajali baada ya mwendokasi wa dereva na kumsababishia
kushindwa kulimudu na kisha kupinduka.
Kamanda Mkumbo amewataja waliofariki
papo hapo katika ajali hiyo ni pamoja na dereva, Moris Lukenza,
Malongo Magongo, Shija Somanga, Yun Somanga, Thobias Simon, Michael
Simon, Amos Lukenza, Shaban Deus na Samwel Malongo wote wakazi wa
mkoani Geita.
Aidha, amesema katika ajali hiyo
kulikuwa na majeruhi sita ambao hali zao zimeelezwa ni mbaya na
kuwahishwa hospitali ya rufaa bugando jijini Mwanza.
Kamnada Mkumbo ametoa wito kwa
madereva mkoani humo, kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa
lengo la kuepukana na ajali zisizo za lazima.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake