Friday, August 14, 2015

PICHA: YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA UKAWA MKOANI MBEYA LEO

 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akiwapumbia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014. Mh. Lowassa na Mgombea mwenza wake Dkt. Juma Haji Duni, walikuwa jijini humo kwa ajili ya zoezi la kutafuta wadhamini wa Tume na kutambulishwa kwa wananchi. Picha na Othman Michuzi
 
Umati wa watu wakiwemo wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA ukiwa umefurika 
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" akimueleza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dkt. Juma Haji Duni akiwahutubia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe akipunga mkono pamoja na wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.










































































9 comments:

  1. Chaguo letu wanyonge tutakupa kura zetu
    Umesemwa sana kutukanwa sana kisa upo Ukawa Tanzania is ya CCM pekee
    Watanzania tunataka mabadiliko na madaliko yako ukawa
    Hata nchi walizotutawala wana serikali za umoja
    Ukawa mungu ibariki

    ReplyDelete
  2. Na hilo gharika katoka nalo Arusha?,na kwa taarifa yenu watu wamejiandikisha kupiga kura,mwamko ulikuwa mkubwa sana wa kujiandikisha katika mikoa yote mikubwa na wilaya zake,lazima mkae.

    ReplyDelete
  3. Haki, nyie mungu Mkubwa, unajua alitakalo linatokea. Haki watanzania wenzangu, make sure those Vote machine they valid , has valid calibration , and also make sure they dont have this called Window CCM!!!!!!!! cause these CCM they know what time it is!!!!!!!! . We tied with these bull shit party run for almost decade and children dont have teachers, school system horrible e.t.c and this year God will panish them!!!!!!

    ReplyDelete
  4. UKAWA OYEEEEEEEE!!!!!!

    ReplyDelete
  5. mnyonge ndio kitu gani?????!!!!

    ReplyDelete
  6. Mnyonge ni
    August 14, 2015 at 10:16 PM
    Anonymous Anonymous said...
    mnyonge ndio kitu gani?????!!!!

    August 14, 2015 at 10:28 PM

    Nk watu masikini
    Ambao tumetumiwa na CCM kwamiaka mingi
    Tu wala hoi
    Tumechoka na zawadi za khanga na vitenge
    Kama khanga hata Ukawa tutapata vile vile
    Tunataka mabadiliko Tumechoka Tumechoka
    Hatumtaki CCM wala Magufuli
    Tunaichukia CCM Kama hitler,au ukoma

    ReplyDelete
  7. mmmmmhhh hivi huyu lowasa si alikuwa ccm??!!! au ni majina tu yamefanana?? kama ni yule wa ccm sasa atasimamia mabadiliko yapi wakati yeye akiwa mbunge wa monduli alipiga kura ya kukataa mapendekezo ya katiba mpya, pia alipiga kura ya kukataa vyama vingi mwaka 1992. wewe unayejiiita mnyonge muulize papa hilo swali kabla ya kuanza kutokota pumba!!! na si ndio huyo aliyelimbikizia mali za mabilioni ambazo kwa mshahara wake hawezi juwa na hata 1/16 ya hizo mali.

    ReplyDelete
  8. MMM cha muhimu ,tuombe Amani ,aijalishe CCM AU Chadema ,tunataka kiongozi bora ,wakishinda,CCM watakuwa wamejifunza,kwa sababu wamepata kashi kashi,wataongopa,wakishinda chadema nao,watakuwa wanaelewa,kuomba tu Amani.mwaka huu sio mchezo uchanguzi shedaaaaaa.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake