Friday, August 7, 2015

UWT YAANZA VIKAO VYA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE VITI MAALUM KUPITIA CCM

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania iliyo chini ya Chama Cha Mapinduzi CCM, imeanza vikao vya uteuzi wa wanaogombea ubunge viti maalum huko makao makuu ya CCM Dodoma. Mkutano huo unaongozwa na mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sophia Simba. Pichani Baadhi ya Wapambe wa Wagombea kupitia Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Mapinduzi (UWT) wakipita na mabango yenye picha za Wagombea wao nje ya ukumbi wa mikutano wa NEC Dodoma kabla ya kuanza mkutano wa uchaguzi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania ya CCM, (UWT), Sofia Simba (katikati) akifungua mkutano wa uchaguzi wa Wabunge wa Viti Maalumu kupitia Chama hicho makao makuu ya CCM mjini Dodoma, kushoto ni Mkamu mwenyekiti wake Asha Makame na Katibu Mkuu, Amina Mkilagi.
Baadhi ya Wajumbe wa mkuatano Mkuu wa UWT CCM wakiwa ndani ya ukumbi wa mikutano wa NEC

1 comment:

  1. Back CCM kwa kiwa umepokea mlungula huna agenda mpya ni kuwa huliwa na mwelekeo.. Salimia.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake