ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 24, 2015

WATU WASIOJULIKANA WAVAMIA NA KUBOMOA NYUMBA YA MGOMBEA UBUNGE CUF MTWARA.

Kundi la watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia na kuibomoa nyumba ya mgombea ubunge wa chama cha wananchi CUF jimbo jipya la nanyamba wilaya ya mtwara vijijini, twahiri saidi baada ya kushindwa kurudisha fomu ya ubunge na kutokomea kusiko julikana huku simu zake za mkononi zikiwa hazipatikani.

Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya viongozi wa chama hicho na wanachi wa jimbo la Nanyamba wamesema mazingira aliyotoweka mgombea huyo  yanaonyesha wazi  kuna mchezo mchafu umefanywa ili kutoa fursa kwa  mgombea wa CCM Abdallah Chikota  kupita bila kupingwa katika jimbo hilo.
Akizungumzia tukio hilo katibu kata wa CUF kata ya Milango Minne eneo analotoka mgombea huyo, amesema mwisho wa kuwasiliana na mgombea huyo ilikuwa majira ya saa saba akimuhimiza kuwahisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi.
Hata hivyo anasema majibu ya mgombea huyo yalionyesha wazi kuna jambo baada ya kudai hawezi kuacha ajira yake na kuingia kwenye kinyang’anyiri cha uchaguzi wakati viongozi wa CUF taifa walimuaidi kumpa shilingi milioni 30 kwa ajili ya uchaguzi na wameshindwa kufanya hivyo na baada ya maneno hayo simu zake hazikuweza kupatikana mpaka muda huu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya maji wa nanyamba oscar ng’itu ambaye aliongozana na mkuu wa kituo cha polisi nanyamba alitembelea nyumba iliyobomolewa na kutoa agizo kwa wananchi kuwataja watu waliyohusika na tukio hilo vinginevyo mkono wa sheria utachukua mkondo wake.


No comments: