MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.
Bi. Samia Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Alisema kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.
Alisema viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika, jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.
Akizungumzia miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk. John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.
Hata hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na vijijini.
Ziara ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM, inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga wakimsubiri mgombea mwenza wa urais, CCM, Bi. Samia Suluhu. |
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenza, Bi. Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi (hawapo pichani) katika Kijiji cha Maguu, Wilaya ya Mbinga. |
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao ni wenyeji wake mkoa wa Ruvuma. |
6 comments:
Hizi ahadi sasa muone hata aibu kuzisema tena mumuogoppe na mungu, si kwa kuwadanganya hivi wananchi wenu hata km ni wapumbavu na malofa hawafikii kudanganyika kirahisi namna hii, hiki chama kilikuwa madarakani zaidi ya miaka 30 mbona hizi ahadi hazikutimia nazilikuwa ziadiwa, miujiza inataka kufanya leo hadanganyiki mtu hapa kabisa labda haoooooooooooo. mungu ibariki tanzania
Juzi ilikuwa maisha bora kwa kila mtanzania leo wamekuja na nini vile!!!!!!!!!!!hakika ni wepesi wa kusahau ila majuto ni mjukuu
Usimhukumu Magufuli & Samia kwa mapungufu ya Kikwete & Lowasa/Pinda. Rekodi zao za utendaji kazi ni tofauti.Give them chance na uwakumbushe 2020
Bwana Mhariri pamoja na vumilia yetu ya matusi katika blog yako kwa kweli sasa inaanza kufikia kikomo. Tulidhani uliianzisha blog hii kwa ajili ya kutupa fursa ya kuelimishana juu ya uchaguzi na viongozi wetu wanaotaka tuwachague. Bahati mbaya kuna wenzetu sasa wameamua kutumia lugha ambayo inatufanya wengine tuanze kusita kuendelea kuisoma. Najua kila mchangiaji ana mtu wake anataka achaguliwe hata hivyo siyo vizuri kutusi wale ambao hawaafiki na chaguo lake. Hivyo ingekuwa busara kama wote tungebakia katika wigo ulilopendekez la kuchangia bila kutumia matusi. Na kama bwana mhariri umeamua kila kinachoandikwa hata haya matusi yachapishwe basi tueleze ili na sisi tujue. Tofauti zetu za kichama au sera zisitufanye Watanzania tuanze kuchukiana.
Lakini ccm utendaji wao upo kamati kuu watu wale wale style ile ile hata skins yesu, mtume muhad, hata Obama kuongoza CCM
Hakuna jipya watanzania tumechoka na kauli zile zile nothing happened to us
Nilifikiri kwenye kampeni zenu mgetueleza jinsi gani mgeboresha maisha yetu
Badala yake kila kukicha Lowassa Lowassa Sisi tutaichi kwenye ninyi kwa kukashifu Lowassa
Mmeishiwa sera CCM
Lowassa ndo chaguo letu
Kama hivyo ndivyo,huyo Lowasa ametoka kwenye the same background tena with the worst ethical rating.
Post a Comment