Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amejitokeza leo na kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa wiki moja iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Askofu Gwajima amekanusha tuhuma za kuwa alimwambia Dk Slaa kuwa wapo maaskofu ambao walihongwa na mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa na kuitwa mshenga wa mgombea huyo.
Askofu huyo amesema kuwa hajawahi kumwambia Dk Slaa kuwa maaskofu wa Kikatoliki wamehongwa na Lowassa ili wamchague hivyo aliyoyasema Dk Slaa ni kuwachafua viongozi hao wa dini.
Wakati Dk Slaa anatangaza kustaafu siasa Septemba Mosi, alimwita kiongozi huyo wa Kiroho kuwa ni mshenga wa Edward Lowassa kwa Chadema na kusema kuwa askofu huyo alimwambia kuwa wapo maaskofu 30 wa Katoliki wamehongwa na Edward Lowassa.
Licha ya kukanusha tuhuma hizo, Akofu Gwajima amesema kuwa kuna watu wanawatumia Dk Slaa na mchumba wake, Josephine, na kuwaonya waache kutumika.
Pia Askofu Gwajima ametoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa kuwa wanatumika pamoja na Dk Slaa.
“Mimi najua wapo Usalama wa Taifa ambao wanamlinda Dk Slaa lakini nawaomba sana Usalama wa Taifa walinde nchi ikae kwa amani, wasijiingize kwenye siasa au kulinda kikundi flani’’ alisisitiza Gwajima.
Aidha askofu huyo amesema kuwa kama Dk Slaa atajitokeza kumjibu kwenye vyombo vya habari, na yeye atajitokeza kuelezea mambo aliyoyafanya Dk Slaa Afrika ya Kusini akiwa na vijana wa Usalama wa Taifa siku chache kabla ya kutangaza kuachana na siasa.
Kiongozi huyo wa Kiroho amewataka wananchi waangalie ni mtu yupi anayefaa na wasije wakagawanywa na harakati zinazoendelea.
CHANZO: MWANANCHI
huyu mchungaji inabidi serikali imnyang'anye kibali cha kuendesha kanisa. kumbe yeye anajishughulisha na mambo ya siasa. kama ni mkweli basi atoe huo ushahidi wa dr slaa akiwa south Africa na usalama wa taifa. kauli zake ni hatari sana na zinaleta uchochezi katika taifa. iko wapi sharia ya mitandao, serikali kafanyeni kazi msimuogope mtu. yeye kazi inatakiwa kuwalisha watu kiroho sasa yuko majukwaani anaendesha chuki na uzandiki na unafiki. sijui mchungaji wa nani na nani anayewachunga kama kauli zake ndio za kipuuzi namna hii. kama kanisa limemshinda aache sio kutuchafulia hali ya hewa.
ReplyDeleteMdau asante ila ukifikiri sana na wewe uko kwenye mtizamo wa kuchunguzwa kwani unatoa kauli za matusi. U najua Tanzania haijweka sawa katiba yake na ndio maana hata hili swala la sheria za mtandao limelazimishwa na serikali yenyewe yenye bunge lao kulinda haki zao kuelekea uchaguzi mku lakini bado haiko sawa na itawaonea wengi! Mtanzania anaruhusiwa kutoa yaliyo moyoni mwake kama Mkapa alivyozungumza jangwani hivyo hana wa kumlaumu. Tusonge mbele tupate kiongozi atakayebadili mwelekeo wa katiba ya Tanzania.
ReplyDeleteMchungaji Ngwajima anapaswa kuchagua mmoja kumtumikia bwana au kujihusisha na siasa moja kwa moja .Serikali inapaswa kuwamulika watu kama Ngwajima wanaochanganya siasa na dini kabla madhara makubwa hayajatokea.
ReplyDeletetatzo wabongo hampendi kuambiwa ukweli,,,, ila ukiambiwa unafiki ndo unakubali.... jaribu kuangalia maongezi yaliotolewa na gwajima,,,,, kaa utulie usome kwa makini utajua ni uongo 100% au kuna ukweli asimilia gani..... its simple ... pitia halafu jiulize,,,, weka mapaenzi ya chama pembeni halafu utapata jibu
ReplyDeleteJamaa anajibu ilivyotokea yeye akiwepo,sasa mlitaka aongee nyie mnavyofikiri?au nyie mlikuwepo?,dr slaa ni mnafiki na hawezi kufurukuta kwa mkewe na chadema walifanya la maana kumtosa sababu siku zinavyozidi kwenda ndio utamjua ni mtu wa namna gani.
ReplyDeletehahahhahhaha kali sana, eti mlinzi aliingia kupitia mlango wa jikoni kumfungulia na kugonga chumbani kwa mama, kwani dr slaa ni kipofu hajui kilipo chumba??? yaani mtu nyumbani kwake hana ufunguo inakuingia akilini wewe mtanzania. gwajima good try mchungaji wa nini tena????!!! this guy is a joker. sijui hao anaowachunga hawajui kupambanua mambo
ReplyDeleteMchungaji Ngwajima kama kweli kuna mambo Dr Slaa amefanya huko South Africa kwa kushirikiana na watu wa usalama unaosema unawafahamu na kama mambo haya ni mabaya na labda yanahusu usalama wa taifa letu unaona tabu gani kuyataja mapema badala ya kungojea hadi baadaye. Mbona mwenzio hakusita kuyataja yale aliyosema ulimwambia kuhusu Lowassa kutoa hongo kwa Maaskofu iliwamchague!
ReplyDelete