Wednesday, September 30, 2015

Kikongwe miaka 100 amtabiria magufuli


Kikongwe, Kete Abdallah

Dustan Shekidele, Morogoro.

UTABIRI! Wakati taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali zikitoa matokeo ya utafiti katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu mwezi ujao, kikongwe mmoja, Kete Abdallah mwenye umri wa miaka 100, amemtabiria ushindi mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.


Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.

Bibi huyo alitoa utabiri huo wiki iliyopita wakati wa sherehe yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa iliyoandaliwa na wajukuu na vilembwe wake na kufanyika nyumbani kwake, Ukonga jijini Dar es Salaam.Mmoja wa wajukuu zake, Dustan Shekidele ambaye ni mwandishi wa gazeti hili, alisema alimkuta bibi yake akiwa amelala kitandani akiwa amekumbatia redio na alipomuuliza sababu ya kuwa hivyo, alidai anafuatilia habari za mgombea huyo, kwani anaamini atashinda na endapo ataamka salama siku hiyo, atampatia kura yake ya ndiyo.

“Unajua ukubwa dawa, najua kila mtu ana chama chake siwezi kuwaingilia, lakini ninawashauri viongozi wangu wa CCM, uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu, upinzani umekuwa na nguvu,” alisema bibi huyo na kuwashauri viongozi wa CCM kutembelea majumbani na mahospitalini kuwabaini makada wa CCM ambao hawataweza kutoka kwenda kupiga kura.

Mmoja wa vilembwe wa bibi huyo, Tumaini Shekidele akisoma risala kwenye sherehe hiyo, alisema bibi huyo alizaliwa Septemba 27, 1915 katika Tarafa ya Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga na kwamba hadi sasa ana wajukuu na vilembwe 302.

4 comments:

  1. Ha a lake Jambo bi mkora huyu
    Kapewa mshiko huyu
    Chezea CCM wewe
    Wetu
    Lowassa
    Lowassa

    ReplyDelete
  2. Huyo aloyemshikilia hapobona kaficha uso wake na kuonyesha nusu. Katumwa kumpandikia huyu kibibi ambaye hata kwenye box la kura haendi. Tumeshtukia mbumu hizi!! Kalagabaho.!!

    ReplyDelete
  3. Hihihi! mara kifimbo. Butiama mara utabiri, hapa hakuna uchawi tena, watz bana eti kalembwa ili apigwe picha

    ReplyDelete
  4. Pamoja na yote hayo CCM Ikulu tena 2015. CCM Oyeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake