Niwape mfano- mimi, Leila, ningekuwa nagombea ubunge Tanga iwe mjini; Korogwe; vijijini; jambo la kwanza, hata kabla sijachukua fomu za mgombea na kujaza, ningekwenda kuwaona wazee wa Tanga.
Wazee wa Tanga wapo Waislamu, tena wa usharika wa Sunni; Shia; Bohora; Ansari Sunna; Ismaili. Wazee wa Tanga pia wanajumuisha Viongozi wa madhehebu ya Katoliki; Anglikana; Luteri; Sabato; TAG; Coptic (Tanga walikuwepo wagiriki). Makanisa mapya hayapendwi Tanga, sijafanya tafiti kufahamu kwa nini.
Baada ya kuwaeleza, na wao kunipa sapoti, ningekwenda kuwaona akina mama wa Miji Kenda, hizi ni familia zinao trace ancestry centuries back, nao pia wanipe sapoti.
Afu, ningekutana na AZAKI; Vijana; WAVIU; Walemavu nk, wote niwaambie azma yangu. Baada ya hapo ndiyo ningejaza fomu.
Tukumbuke kwenye mikasanyiko yote ya watu ni sehemu ya kupatia wapiga kura.
Mimi Tanga ningefanya zeffe, na matwari; afu ningezungushwa na Wazee wa madhehebu yote kwenye gari au bajaji iliyowazi na kutambulishwa upya. Tena mungeniona navaa ushungi kabisaaa.... Tanga hata Wakristu wanavaa hijab au baibui.
Niongezee kwa kuwaweka jumuiya ya Hindu- wapo wengi Tanga, mungeniona kwenye luninga nimevaa gagri choli napiga vikengele huku naimba Om, Jagdish, Hare, Swami Om, Jagdish, Hare, kwenye Mandir afu mungeniona Guruduwara kwa Sikh (Singh) community, ndani ya hekalu nimevaa kurta na Patiala, naimba "Ek Omkara.....".
Baada ya hapo mungeniona kwenye tambiko la wa Seute- Wabondei; Wasambaa na Wazigua; na wafaume akina Shekimweri; Pongo; na akina Zumbe Mang'enya wakinirushia maji kwa usinga wa nyumbu, huku nimevaa kaniki 3 na majivu usoni. Ningeitwa kwa title yangu yaki Seute Nemganga Mmasoa.
Ni mkakati wa kampeni.
Mhe Lowassa na Mhe Magufuli na Dada Anna, ooh! na Lyatonga- nasikia anawania urais, wanayo hiyo haki ya kuwaomba Watanzania kuwapa kura yao, hata ikiwa wamekutana kwenye public bathrooms.
Waswahili tuna usemi "Umwonapo Zumbe, ndiyo unamwamkia". Mimi nasema, "Let them fly. Let them campaign. Let them tell us their Vision. Let them tell us what they would do if we gave them the responsibility of being our servants and how they intend to serve us, so that we, the owners of this beautiful Tanzania, benefit from their service. That we feel safe and secure in our country. That they would not use coercive and harmful and oppressive methods to cower us into subjugation; into fear; into poverty when they, are in our service".
Hallelluya!
Leila Sheikh
It's true
ReplyDeleteMimi mwislam
Awamu ya pili marehem malima aliweka maafisa elimu wilaya hadi mkoa waislam ili wawakombowe waislam
Na kipindi hicho wazir I Fatuma Said nilimskia kwa mdomo wake akisema waislam walionewa enzi za mwl
Sasa ni enzi zao wakati akikaa magogoni
Nape ulikuwa kinda wakati huo
Ni upuuzi katika ubora wake!
Deletewee anonymous wa 8:31 sio mwislamu bali mnafiki wa mitaani kwenda zakoo huna mpya uzushi tuu. miskitini na makanisani ni mwahala mwa ibada na sio kampeni za kisiasa. ndo nyinyi baadae mnatuletea mitafaruku ya kidini acheni kutetea upuuzi huu kidini.
ReplyDelete