Tuesday, September 8, 2015

LOWASSA AINGIA KATIKA TUHUMA ZA UDINI BAADA YA KUSEMA HAYA VIDEO

9 comments:

  1. Kawaida kwenye siasa
    Mbona mkapa aliita watu wapumbavu na malofa
    Lakini kasema kanisani tena kwa uwazi
    Mimi ni mwislam najua tangu awamu ya pili jinsi gani waislam walivyokuwa na mikakati na awamu ya nne
    Lakini lowassa mbona msikitini anakwenda kuchangia harambee mite sion Dili hi lakini ccm wamaivaliya njuga
    Kuna kijimage kipo USA sijui kamkosea nini Lowassa tangu yuko ccm kamtukana matusi ya ajabu sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lowassa aliongelea Walutheri kwamba wao mbona hawapati urais? Hakuongelea wakristo au waislam. Anaamini kwamba kila dhehebu lazima litoe rais kwa zamu.. Siyo dhambi lowassa kuamini hivyo

      .. Kikwette amefanya hivyo, MF. Waziri mkuu kutoka Sumbawanga, Rais wa Zbar kutoka Pemba, Waziri wa fedha kutoka Zanzibar, nk.
      .. Ipo haja ya kuangalia jamii yote ktk mambo haya ya uongozi wa nchi...

      Delete
  2. Hivi kweli mtu akizungumza na waumimi wenzake na kuwaomba wamuunge mkono tayari tuhuma! Hakuna udini wwowote ni basintu UCCM umejaa.

    ReplyDelete
  3. Nimekuwa nikifuatilia mielekeo ya kisiasa ya viongozi wa CCM na watoto wao pamoja na watu wao wengine wa karibu kinasaba, na kushuhudia kuwa, ukiacha viongozi wenyewe wa CCM, kundi la pili ambalo linafanya kila kinachowezekana kujaribu kukinusuru chama hicho ni la watoto wa viongozi hao. Wapo watoto wengi wa viongozi wa CCM, hasa katika magroup ya WhatsApp na mitandao ya kijamii, wanapigana kufa na kupona kunusuru ulaji wa wazazi wao.

    Kete yao kubwa ambayo wanaitumia kuonyesha umma kuwa upinzani haufai ni kuwa "Lowassa ni fisadi". Wengi wamejitoa ufahamu, wana uwezo mdogo wa "kureason" unaoambatana na kuchanganyikiwa, na hoja wanazojenga wakati wa malumbano ni za kushangaza mno!

    Hutaamini majibu, ushindani na hoja zao pindi utakapokutana nao na kujaribu kuwaeleza kuwa tulipofika kuna haja ya mabadiliko!

    Hoja zao zinatia hasira vibaya sana na kuashiria kuwa wao wana hatimiliki ya hatma ya Tanzania.

    By LifeHacker/JF

    ReplyDelete
  4. Ikumbukwe katika katiba ya Tanzania, nchi yetu haina dini hivyo basi kila muumini ana haki ya kuchagua dini yoyote ile. Lowassa amaetumia nafasi yake kama mwananchi kutoa mtazamo wake wa kidini na sidhani kama inaonyesha ubaguzi wowote ule. Mbona Nape hakuandika barua kukemea mauaji ya kidini yaliyokuwa yakijitokeza?

    ReplyDelete
  5. kama kawaida yake huyo hanaga jipya zaid ya kuropa tu. nape tunakujua vema. ahsanteni sana watoa maoni hapo juu, ni kweli kabisa mauaji ya kidini nape alipiga kimya, matusi ya mkapa ya hadharani kimya, ya Mh Lowasa imemkuna, hapo mnajidhihirisha ni jinsi gani mmekata tamaa, mmemchafua kwa kila namba, hata mkadiridi kuwanunua viongozi wa UKAWA vyote hivyo havikusaidia wananchi kurudi nyuma, sasa umeibuka na lisilokua na tija kabsaa, eti siasa za udini, una jipya wewe, kwanza wananchi hawataki hata kukusikia kwa taarifa yako, huna aibu eti udini? mauaji,matusi ukuyaona au kuyasikia? Lowasa tunampenda kwa mahaba. Lowasa oyeeeeeeeeeeeee.
    Ikulu wazi kwa ajili ya Lowasa.

    ReplyDelete
  6. mskilizeni vizuri Lowasa, mapenzi tuweke kando. "Nyerere alikuwa mkatoliki, Mkapa alikuwa mkatoliki" hivyo huu ni wakati wa walutheran kumpa kura zaidi ili ashinde, ushindi wake ndio ushindi wa walutherani. shame on him!!

    ReplyDelete
  7. sera sera sera,kama huna sera nenda hata kwa baba baba askofu wa kkkt #hapa ni kazi tu, ukawa bado hamjaona rangi. oooooh mimi mlutheri, ooooh mimi mmasai, oooooh mwenyekiti wangu mchaga nipeni kura zenu!!!!!! mambo hao kafanyeni ndani ya chama chenu kuchagua viongozi wenu sio kwa watanzania kuingia ikulu

    ReplyDelete
  8. Vyama vyote vilipewa na kusoma kanuni na sheria za Tume ya Uchaguzi (NEC) na viongozi wote wa vyama walikubaliana nazo na ndio maana wakatia sahihi. Moja ya hizo walizotilia sahihi ni kutoendesha shughuli za kampeni kwenye nyumba za Mungu. Tatizo hapa liko wapi? Kama kiongozi kakosa lazima tukubali kuwa amekosa. Kama kuna yeyote ambaye alikuwa hakukubaliana na hili angeiiongea walipokutana kwenye Tume na kulijadili.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake