Wednesday, September 30, 2015

MWIGULU NCHEMBA ATUA KWA MBOWE NA MBATIA,SAME NA MWANGA...CCM YAENDELEA KUSAKA KURA KATA KWA KATA

Wananchi wa Hai Mjini wakimpokea Mwigulu Nchemba kwa shangwe.Mwigulu Nchemba ameshawasili Hai Mjini kuzungumza na Wananchi na Kumuombea Kura Rais Mtarajiwa kutoka Chama cha Mapinduzi Ndg,J.Pombe Magufuli.Mwigulu Nchemba akitoa Darasa kwa Wananchi wa Hai Mjini kuhusu Umuhimu wa Kuchagua kiongozi kwa Malengo,sio kuchagua Uongozi kwa Kishabiki."Wanahai naomba Mmchague Magufuli kwasababu ndiye kiongozi anayeweza kushughulika na Matatizo ya Wananchi wetu hasa swala la Rushwa,Uzembe maofisini na wadhurumaji.Kwa hapa Hai mmeshaonja ubaya wa Upinzani,hawajishughulishi kwa maendeleo Zaidi ya kupiga kelele zisizokuwa na tija kwa Wanahai".Wananchi wa Hai wakisema Nguvu Moja.Mwigulu Nchemba akiwasili USA river hapo jana.Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa USA River mapema hapo jana.Mbunge mtarajiwa wa Moshi Mjini Ndg.Davis Mosha akisalimiana na Mwigulu Nchemba wakati wa Mkutano wa hadhara ndani ya kata ya Sokoni.Mwigulu Nchemba akimnadi Davis Mosha mbunge Mtarajiwa kwa Moshi mjini.Mwigulu Nchemba akiwasili Same Mashariki.Mwigulu Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Same Mashariki Bi.Anna Kilango Malecela mapema hii leo wakati alipokwenda kuinadi Ilani ya CCM.Comrade Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Same Mashariki kuhusu Umuhimu wa kufanya Uchaguzi kwa Amani,Pia kuichagua CCM kwasababu imefanya kazi kubwa kuiletea Maendeleo Nchi yetu,Kwa Same serikali ya Magufuli nakwenda kujenga Barabara kwa kiwango cha Rami kuelekea Nkomanzi na Same Mashariki.Wananchi wa Mwigulu Nchemba akimndai Mathayo David Mgombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi.Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Vunjo kupitia CCM Ndg.Innocent Shirima hii leo.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Vunjo kuwa Mabadiliko sio vyama,Mabadiliko ni shughuli za maendeleo na Utendaji kazi.Magufuli anakwenda kubadilisha Utendaji kazi na Usimamizi wake.
Picha na Sanga R.

7 comments:

  1. Mwigulu. Kwanza tueleze fedha za mikopo ya wanafunzi ulizifanyia nini ukasubiri waandamane na keshoye ukaziweka wazi. Unaonekana kuwa mzigo mkubwa kwa serikali na wananchi wake. La msingi kupumzishwa kwanza waache wenye nia ya kuleta mabadiliko. Sio ndani ya hili chama unachotetea!!.

    ReplyDelete
  2. Watu wa kuunga unga hao
    CCM Kama wanawake
    Wanaume wazima ovyo
    Hai si vunjo
    Hampati NGO
    Nenda iramba kwa wanyira via wenzio

    ReplyDelete
  3. Hakuna aliyerudisha kadi chezea Kilimanjaro
    Wewe

    ReplyDelete
  4. Oops kampeni zenu zina walenga Watu na sio sera zenu
    Mmechoka mwili hadi akili

    ReplyDelete
  5. Hamna Mtu wa Hai hapo

    ReplyDelete
  6. CCM oyee!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Nyinyi andikeni mnalotaka, tukaneni mnavyotaka lakini 10/25 ni kikomo chenu. CCM itachukua tena madaraka na Ukawa yenu, kama itaendelea kuwepo, itakuwa Ukiwa!!!!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake