ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 15, 2015

Flyover ya TAZARA kuanza kujengwa mwezi ujao

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kulia) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SUMITOMO MITSUI, Bw. Ichiro Aok kutoka Japan wakiweka saini Mkataba wa kuanza ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika eneo la TAZARA.  SUMITOMO MITSUI ni kampuni iliyoshinda zabuni ya kujenga barabra hiyo, ambao ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Novemba 2015 na kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu.  Wengine katika picha waliosimama watatu kutoka  kulia ni  Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, kushoto kwake ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida na Mwakilishi Mkazi wa JICA nchini Tanzania. PICHA NA: REUBEN MCHOME.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kulia) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SUMITOMO MITSUI, Bw. Ichiro Aok kutoka Japan wakibadilishana mikataba baada ya kuweka saini.
Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiongea kabla ya uwekaji saini kukamilika. Dkt. Magufuli alieleza kuwa barabara hiyo itakapokamilika itakuwa ni ya kwanza ya aina yake katika nchi za Afrika Mashariki.

Mshauri mwelekezi wa kampuni hiyo Bw. Keigo Konno akionyesha jinsi mradi huo utakavyokuwa huku Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akifuatilia 
Sampuli ya barabra ya juu ya TAZARA itakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika.
Barabara ya juu
Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akiteta jambo na Balozi wa Japan hapa nchini.  

12 comments:

Anonymous said...

Asante kwa taarifa nzuri japokuwa tunamaliza kampeni tunaomba yeyote atakayekuwa kwenye Serikali ijayo bila kujali nani ahadi hii itekelezeke issije ikawa ya miaka mitano kwenda kumi ijayo!! Tumesikia mengi saana kwenye hizi kampeni hadi umeme vijijini wakati mitambo ishazimwa!! amani Tanzania.

Anonymous said...

Mdau tunakushukuru kwa kutujulisha hili. Lakini hiyo video ilowekwa na yale majengo tunayoyajua ya hii barabara sijui kama kweli inakuja vipimo vyake!! isije ikawa ndio kiini macho kwa ajili ya kuelekea uchaguzi kwani haya mambo yalikuwa yawepo miaka 15 iliyopita!! tarehe zilizotajwa sio mbali na uso wa Tanzania ya leo!!

Anonymous said...

Hizi kampeni CCM
Wadangayika hatudanganyiki ngoooooooooooooooo

Anonymous said...

Hiii ni kampeni Kabisa
Huyu ni mgombeaji urais iweje awe hapa
Shame you CCM
Lowassa Lowassa it's our choice

Anonymous said...

Kenya zipo kibao

Anonymous said...

Nimeiangalia hii video vizuri mbona hao wa Nelsoni Mandela rd bado wana traffick light wa Julius Nyerere rd tuu ndio wanaoweza kupita through

Anonymous said...

Kwa hiyo,kama Kenya ziko kibao hatupaswi kuwa nazo?

Anonymous said...

Watanzania tumekuwa watu wa ajabu sana,mkiwa hamna mnapiga kelele mwekewe,mkipewa mnalalamika..It doesn't matter kama huu ni mkakati wa CCM au laa,.At the end of the day, tutakuwa tumepata huduma..

Anonymous said...

Pamoja na haya yote ukweli ni kuwa maendeleo ya nchi hayapatikani siku moja hivyo tunawapa hongera wote wanaojitahidi kutuletea maendeleo haya hata kama hayakidhi matakwa ya kila mmoja wetu. Ikumbukwe kuwa sisi wote ni binadamu na kila binadamu ana utashi wake. Hata hivyo mpaka hapa hongera sana CCM na wengine tunaoona kuwa mnajitahidi tuko nanyi hata huu wakati wa mchakato na inshallah tutakuwa tena pamoja 25/10/2015 na bahada ya hapo ili kusheherekea ushindi.

Anonymous said...

DK Magufuli ni waziri wa ujennzi waTanzania na ukweli ni kwamba hakuna kiongozi yeyote Tanzania atakae weza kutoa usimamizi bora na uadilifu wa hali ya juu wa miradi mikubwa ya serikali kama maghufuli. Wajapani ni wataalam wa kutengeneza miundo mbinu ya uhakika kwa hivyo Tanzania imekuwa makini kwa hapo na Daresalam kweli itabadilika cha kuomba hapa magufuli awe raisi kila Kitu kitakamilika kama kilivyopangwa. Sio tushabikie kumpeleka mgonjwa lowasa ikulu watanzania itakuwa tumejirejesha nyuma sisi wenyewe. Na lowasa sio ugonjwa wake bali hata uadilifu wake mashaka sio wa mtu wa kumkabidhi kusimamia rasilimali zetu za nchi alipo iba panatosha sasa kazi tu tunaka kupiga maendeleo na kumovu forward.

Anonymous said...

Ha ha ha danganya toto

Anonymous said...

Kubali, usikubali hali halisi ndiyo hiyo na Magafuli ni chaguo la wengi.