Monday, October 12, 2015

LUBUVA - MALALAMIKO YA VYAMA YATATULIWE NDANI YA KAMATI YA MAADILI NA SIO VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva  akizungumza katika mkutano na  vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mkurugenzi wa uchaguzi, Kailima Ramadhan akizungumza na wadau wa vyama vya siasa leo jiji ni Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia maada leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda.

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa  ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amevitaka vyama vya siasa kupeleka malalamiko yao katika kamati ya maadili ya NEC  na sio kwenda kutoa malalamiko yao  katika vyombo vya habari.

Lubuva aliyasema hayo leo wakati NEC ilipokutana na vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,amesema kuwa  nafasi vya siasa vina nafasi ya kuhamasisha watu wapige kura kwa wale wenye sifa.

Amesema wakati wa kupiga kura watu wakipiga kura wanatakiwa kuondoka na kazi zingine zitafanywa na mawakala ndio watakaofanya kazi zoezi la kuhesabu na baadae kubandika.

Lubuva amesema watu wakikaa vituoni wanaweza kuvuruga amani  na kufanya zoezi  la upigaji kura kuharibika.
Amesema tume imejipanga katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika  kwa uhuru na haki kutokana na mfumo  wa kisasa.
Aidha amevitaka vyama vya siasa kunadi sera zao  na sio kushughulika na watu kwani wananchi  wanahitaji sera waweze kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi.

Baadhi ya vyama vya siasa vimeridhishwa na ushirikishwaji wa NEC katika masuala kuelekea uchaguzi mkuu na jinsi walivyojipanga uendeshashaji wa uchaguzi mkuu.

CHANZO: MICHUZI BLOG

4 comments:

  1. Usitishe Watu wewe mzee
    Sheria 200
    Tutajazana kwenye mabaa yote Na nyumba zinazozunguka
    Mwaka hatulali
    Tu anataka matokeo tuyajuwe

    ReplyDelete
  2. Baada ya kuona uelewa wa washabiki wake,Mbowe hakukosea Ukawa mnachohitaji ni " Elimu,Elimu, Elimu".

    ReplyDelete
  3. Sheria zifuatwe hata kama wengine hatutaki.

    ReplyDelete
  4. kailima ni ccm-damu na,sikia,wewe ni mwongo,utaendelea kua muongo,ila kwa hili la uchaguzi mkuu mwaka huu 2015 huwezi kufanya fyoto,utafyotolewa na umma na nguvu za umma,PEOPLES POWER.CCM BYE-BYE.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake