ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 15, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MABITI, DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini Kitabu cha Maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Marehemu, Pascal Mabiti, wakati wa shughuli ya Msiba iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. Pi
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Marehemu Pascal Mabiti, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu marehemu, Pascal Mabiti, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika nyumbani kwa marehemu, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu marehemu, Pascal Mabiti, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika nyumbani kwa marehemu, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015

3 comments:

Anonymous said...

Tunapenda kuwapa pole sana wafiwa kwa kuondokewa na mpendwa wao. Na Mwenyesi Mungu aendelee kuwapa nguvu. Najaribu kupata hii Simiyu iko maeneo gani jijIni Dar Es Salaam!! nyumbani kwa marehemu!!

Anonymous said...

Poleni sana wafiwa. Na mimi nimestuka nafikiri Mkoa wa Simiyu umehamia pande za Upanga. Tanzania bwana!!

Anonymous said...

Simiyu ni mkoa unaojitegemea na wala siyo sehemu ya jiji la Dar es Salaam. Mkoa wa Simiyu ni mkoa mpya unaotokana na kugawanywa kwa mkoa wa Shinyanga kuwa mikoa miwili inayojitegemea. Kabla ya kugagawanya, mkoa wa Shinyanga ulikuwa na wilaya za Shinyaga, Mjini, Shinyanga Vijijini, Kahama, Bariadi na Maswa. Baada ya kuugawa wilaya za Shinyanga Mjini, Shinyanga Vijijini na Kahama zikabaki kama mkoa wa Shinyanga na zile wilaya za Maswa na Bariadi zikaanzisha mkoa mpya huu wa Simiyu.

Kama ilivyoandikwa kwenye habari marehemu Pascal Mabiti ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, alikuwa ana nyumbani yake Upanga, Dar es Salaam na ambako shughuli za msiba zilikofanyika.

Mhe. Pascal Mabiti R.I.P