ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 15, 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI JENGO LA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI DODOMA

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo, tarehe 15 Oktoba, 2015, amelifungua rasmi jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Rais Kikwete ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa kujenga jengo zuri linaloakisi sifa na heshima ya utendaji wa Ofisi hiyo.

Kwa upande wake CAG, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Nne kwa kuiwezesha ofisi yake na kuongeza uhuru wa ofisi hiyo kwa kuwawezesha kujenga majengo katika mikoa ya Singida, Morogoro na Kilimanjaro.

Ufunguzi huo ulishuhudiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, baadhi ya viongozi waandamizi na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kutoka Makao Makuu na Dodoma. Kwa upande wa Wizara ya Fedha walioshuhudia ni Waziri wa Fedha, Bibi Saada Mkuya na Katibu Mkuu wake, Dkt. Servacius Likwelile.

Jengo hili limekusudiwa kuwa makao makuu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambalo limefunguliwa rasmi na Rais Kikwete mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati alipofika kuzindua jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati alipofika kuzindua jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kibao cha uzinduzi wa jengo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kibao cha uzinduzi wa jengo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) kwa pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (kulia) na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma. Kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (kulia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma. Wengine pichani waliokaa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa (kushoto), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (wapli kushoto). Wengine ni Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (wapili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile (kulia).

5 comments:

Anonymous said...

Tanzania ina msago mawili ?
Lini ikulu itahamia Dodoma ?

Anonymous said...

Sorry I mean makao makuu mawili
Dodoma Na Dar Es salaam
How much it's cost to have two capital cities for poor country like Tanzania who depend from our money from Europe
Shame you CCM

Anonymous said...

We European
We can't pay our tax for the country who have two capital cities Dodoma and Dar Es salaam
It's our money we need to knowwwwwwwww it

Anonymous said...

Safi sana Tanzania inapaa. Nashangaa wale wanaoitukana serikali kwa kila kitu ingekuwa vizuri kuipongeza kwa mazuri yake inayoyafanya, demokrasia sio chuki na uadui baina ya taasisi kwa taasisi au mtu kwa mtu. Demokrasia ni kupongezana na kukosoana kwa njia ya amani na kuheshimu mawazo tofauti na yale mtu anayoyaamini ni sahihi. Demokrasia inapo husushishwa na maendeleo katika jamii husika basi hakuna budi kumpongeza yule aliefanya jambo la maendeleo kwa manufaa ya uma hata kama ni mpizani wako kwani huwezi kuimba wimbo wa mabadiliko wakati wewe mwenyewe huna nia ya kubadilika hata kwa kauli hayo yatakuwa sio mabadiliko bali ni upuuzi mtupu.

Anonymous said...

Nimependa sana aliyoandika anonymous wa October 16, 2015. Tofauti kichama au kiitikadi sio uhasama. Hivyo mpinzani wako akifanya mazuri kwa manufaa ya wote anastahili kusifiwa.