DIKTETA NI NANI, NA KWANINI TUNAMHITAJI?
Na Mubelwa Bandio
Na Mubelwa Bandio
January 7, 2009
Photo Credits: Synergy
Ninapoangalia namna "tunavyokaririshwa" maana za nani ni nani, na kwanini ni yeye na kwa manufaa ya nani na nani awe rafiki na nani awe adui yake nasikitika sana. Tumepangiwa kila kitu kwa tafsiri ya wenzetu ambayo kwa hakika ni kwa manufaa yao.
Mandela alikuwa "mkorofi" ( na dikteta fulani hivi) kwa kudai uhuru ambao baada ya kutambulika sasa anaonekana ni shujaa japo hajabadili alichofanya, Saddam alikuwa shujaa aliposhirikiana na wao kisha akawa dikteta alipopingana nao. Gadafi aliyekuwa dikteta na kuonekana kama asiyewajali wananchi wake sasa kawa shujaa na "kiongozi safi" kwa kuwaruhusu "wakuu" kuingia na kukagua silaha zake japo hakuna alichobadili kwa wananchi.
Luciano aliwahi kuimba kuwa "they're trying to control our minds, and treating us like swine. They telling us who to love or hate as if they're great"
Najua akitokea mtu akalazimisha baadhi ya mambo ya maana kutendeka nyumbani basi ataitwa dikteta (na kwa bahati mbaya nasi tutashabikia hata kama si tafsiri yetu).
Najiuliza akitokea "kiongozi" akalazimisha kusimamishwa kwa mikataba yote ya madini ili ipitiwe upya hataonekana dikteta?
Je atakayelazimisha viongozi wakuu waliosababisha mabilioni ya hasara serikalini wachunguzwe licha ya katiba waliyoshindwa kuitii kutosema hivyo hataonekana dikteta?
Je atakayelazimisha wabunge kujenga ofisi na kutumia muda mwingi majimboni mwao kama walivyoahidi wakati wa kampeni hataonekana dikteta?
Atakayelazimisha utendaji wa mikoa kulingana na rasilimali zake kuwanufaisha wananchi wake na kisha nchi nzima huyo hataonekana dikteta?
Najua kuwa atakayewafikisha viongozi wakuu mahabusu ataitwa dikteta kwa kuwa amekwenda kinyume cha katiba, lakini sijui kwa nini katiba imlinde yule ambaye ameivunja kujilimbikizia mali na kuitia serikali hasara kubwa?
Kama huyu atakayetenda haya niliyosema hapo juu, atakayevunja mikataba ya ujenzi wa miundombinu yenye utata, atakayehakikisha ahadi za wananchi zinatekelezwa na waahidi hasa wabunge, atakayeshurutisha matumizi mazuri ya rasilimali za wananchi kwa manufaa ya sehemu husika, atakayeshinikiza malipo kwa wafanyakazi ambayo mpaka sasa haijajulikana kwanini hawajalipwa ilhali waheshimiwa wanapata pesa zao bila malimbikizo, atakayehakikisha kuwa mkulima wa anapata senti zake zote alizoikopesha serikali na ambazo anatumia pesa nyingi kufuatilia kuliko atakazolipwa, atakayesimamisha ziara za nje na ndani za viongozi (zisizo za lazima) na atakayeamua Tanzania iwe ya manufaa kwa wa Tanzania kwa kutumia kila kilichopo Tanzania ataitwa DIKTETA, basi namuombea awepo.
Aje atufanyie hayo na nadhani tunamhitaji na anaweza kuwa suluhisho la awali kwa yaliyopo. Maana sasa imekuwa kama alivyosema Kaka Evarist kuwa HAKI IMEKUWA FADHILA na twahitaji atakayeangalia haki kama haki .
Nionavyo ni kwamba mfumo unaotumika kumpata mtu atayewania uongozi unapita katika ngazi na misaada ambayo mpaka aje kupatikana mgombea anakuwa kashirikisha "wataalamu" wa ufujaji ambao akichukua madaraka hataweza kusema lolote juu yao.
Sasa hivi, hata nchi yangu Tanzania iongozwe na Masia na Mtume, iwapo MFUMO UTAKAOTUMIKA NI HUU ULIOPO, bado upande pekee wa maendeleo tutakaoelekea ni wa MAENDELEO HASI.
Tatizo la Tanzania si watu walio madarakani, bali ni MFUMO unaowaweka pale, unaowaongoza katika kuongoza na unaowawajibisha.
Pengine nionavyo mimi ndilo tatizo, lakini kuna ukweli kuwa tafsiri nyingine zinatufanya tuwachukie wale ambao wanaweza kutuletea mabadiliko ya kweli na badala yake tunaendeleza "kubebana na kufichana" ambako kunaendelea kutuweka tulipo.
Ni Mtazamo wangu tu na naendelea kutunza haki ya kukosea na kukosolewa.

Sioni mauzui yoyote ya maana katika hii mada au labda mtoa mada anatamanio ya kuona Tanzania inaendeshwa kidikteta .
ReplyDeleteUmekasemapo MTANI nina-consign.
ReplyDeleteOk good men.umeandika maoni Mazur Sana.Tumetoka kumaliza uchaguzi Na rais amepatikana tamari, hivyo Mh Magufuli anazo 85%za kutosheleza maoni yako Na hii 15%inayobakia inamezwa Na mfumo wa Chaka kilicho muweka madarakani. Anaonekana kufaa sababu Ni muadilifu,mchapa kazi Na jasiri wa kukemea maovu Na maamuzi yake Ni magumu Sana.
ReplyDelete