Tuesday, November 10, 2015

MAGUFULI KUJA NA WIAZARA 22 TU

Rais Dkt John Pombe Jodeph Magufuli

OFISI YA RAIS [PRESIDENT’S OFFICE]
1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-[Utawala Bora]
2. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais [Menejimenti ya Utumishi wa Umma]
3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais [Muungano, Mahusiano na Uratibu]
OFISI YA WAZIRI MKUU [PRIME MINISTER’S OFFICE]
4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na Bunge]
5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu [TAMISEMI]-
6. WIZARA YA KILIMO, CHAKULA, UVUVI NA USHIRIKA
a. Naibu Waziri (Uvuvi na na uhifadhi fukwe na viumbe maji)
b. Naibu waziri (Mifugo na Umwagiliaji)
7. WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
8. WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
9. WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
10. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
11. WIZARA YA NISHATI NA MADINI
12. WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI
a. Naibu waziri (Sera)
13. WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
14. WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, JINSIA na WATOTO
a. Naibu waziri (Jinsia na watoto)
15. WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
16. WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA, UWEZESHAJI, UWEKEZAJI NA MASOKO
17. WIZARA YA HABARI, VIJANA, AJIRA, UTAMADUNI NA MICHEZO
a. Naibu waziri (Utamaduni na Michezo)
18. WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
19. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
20. WIZARA YA MALIASILI, MAZINGIRA NA UTALII
a. Naibu waziri (Mazingira)
21. WIZARA YA UJENZI
22. WIZARA YA UCHUKUZI

Mawaziri 22
Manaibu 6
Serikali iliyopita ilikuwa na mawaziri na manaibu wake Jumla 66 wakati rais wetu mpya JPM atakuwa na Jumla 28…. Safari za Nje kwa kibali cha Ikulu tu!!

11 comments:

  1. Tanzania nayoitaka naiona ileeeeee inakuja,do your thing Mr President,hapa kazi tu

    ReplyDelete
  2. SIONI WIZARA YA MAJI

    ReplyDelete
  3. Huyu Rais Magufuli Mwenyezi Mungu amzidishie nguvu ya kulitoa hili Taifa la TZ lililokuwa kwenye kiza na shimo refu sana yaani kuunda baraza la mawaziri dogo kama hili inaifanya serikali kuwajibika kikamilifu. yaana anafanya mambo ambayo wengi walikuwa wanadhani wapinzani wangefanya lakini yeye anayafanya kwenye CCM ileile. kodi wa wafanyabiashara wakubwa, afya muhimbli, na sasa mawaziri 22 yaani ananifurahisha kila kukicha hata mwezi hajatimiza Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  4. very interesting - where will he put all those Drs, Professors etc who think politics is the easiest way to accumulate monies. Kama hakuna kula so the next election we hope there will be no candidates at all - Bongoland!

    ReplyDelete
  5. What will he do with the escarow people, they told us $10 million ni za mboga. they are still coming back as MPs. Are they supposed to be there?

    ReplyDelete
  6. We uliyeuliza kuwa huoni wizara ya maji, kwani majirani zetu wanazo?

    ReplyDelete
  7. hivi maji sio nishati eeh?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maji ni nishati pale inapotumika ku generate power,but for the most part huwa katika huduma ikilenga kilimo na matumizi ya watu.

      Delete
  8. Hamna haja ya wizara ya Maji kwa sababu chini ya Wizara ya Kilimo, dept. ya Mifugo na Umwagiliaji, mambo ya maji yanaweza kuwa hapo. Kuhusu mdau aliyeuliza wapi hao Professors na Drs. wataenda, binafsi nadhani the answer is simple: Wajiunge na sekta ya Elimu, wafundishe au wajiunge na Private Sector (nje ya serikali) ambako utaalamu wao utasaidia maendeleo ya nchi.

    ReplyDelete
  9. MAJI: Nadhani maji yako kwenye wizara ya mali asili, mazingara na utalli. kwa sababu maji ynahitajiwa sana kwa maisha bora, afya ya watu na wanyama pamoja na uchumi wa nchi, naona ifunguliwe waziri wake na nyingine zifutwe

    ReplyDelete
  10. Wizara zinaweza kuwa 15 tu, kama nilivyowahi kupendekezwa. Orodha au idadi ya wizara naifanya iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:
    1. Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
    2. Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi.
    3. Habari, Utamaduni na Michezo.
    4. Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
    5. Ulinzi na JKT.
    6. Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; na Sheria (Katiba na Utawala Bora).
    7. Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto.
    8. Afya na Ustawi wa Jamii.
    9. Mazingira, Nishati, Madini na Miundombinu.
    10. Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana.
    11. Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika.
    12. Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko).
    13. Kilimo, Ushirika, Uvuvi na Mifugo.
    14. Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge; na Mambo ya Ndani na Uhamiaji.
    15. Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia.
    :

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake