Mke wa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, Regina Lowassa
Mke wa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, Regina Lowassa, ameikataa nafasi ya ubunge wa viti maalum aliyopewa na kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani.
By Mwandishi Wetu,
Mke wa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, Regina Lowassa, ameikataa nafasi ya ubunge wa viti maalum aliyopewa na kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani.
Kwa mujibu taarifa wa kutoka familia ya Lowassa, Regina anaichukulia kwa heshima kubwa nafasi hiyo, lakini anaamini ataweza kushughulikia matatizo ya akina mama na watoto akiwa nje ya Bunge.
"Naishukuru kamati Kuu ya chama changu kwa heshima hii kubwa waliyonipa na ninaithamini sana, lakini naamini nitaendeleza mapambano ya kuwaletea akina mabadiliko kwa ufanisi zaidi nikiwa nje ya bunge," amesisitiza mke huyo wa waziri mkuu wa zamani katika taarifa hiyo.
Kamati Kuu ya CADEMA ilifikia uamuzi wa kumpa Regina nafasi ubunge viti maalum kutokana na mchango mkubwa aliyoutoa wakati wa kampeni ambao kwa kiasi kikubwa ulisaidia upatikanaji wa majimbo mengi tofauti na uchaguzi wa mwaka 2010.
Chanzo: Mwananchi

Amefikia conclusion kwamba CHADEMA is ideologically defunct. Haoni faida iliyopo kubaki Chadema. Guess who is next on the exit door? Fisadi himself.. stay tuned!
ReplyDeleteMchangiaji ungesoma statistics za upward progress ya chadema nadhani ungetafakari ni namna gani uandike. CDM is becoming stonger and CCM is loosing grips. Kaa mkao wa kula 2020 utapata hasira zaidi. Pole sana.
ReplyDeletengoja nijichukulie popcorn zangu na soda yangu ya cocacola movie imeanza.
ReplyDeleteMama anaulizia chenji yake in hard currency, wao wanataka kumlipa kupitia ubunge.
ReplyDeleteHawa (mr&mrs Lowassa) interest yao siyo CHADEMA! Walitaka kutumia hiki chama (chadema) kama platform tu yakufanikisha mambo yao. Kama kweli huyu mama angekuwa na mapenzi na hiki chama asinge-reject hiyo offer ya ubunge wa viti maalumu. Kama alivyodokeza mchangiaji hapo juu, sitashangaa mzee mzima (EL) naye akijiengua Chadema kwani anaonekana wazi kuto-fit in kwenye company ya akina Mbowe na wenzake.
ReplyDeleteNakuunga mkono wewe uliyeandika last comment in this page. Mr & Mrs Lowassa hawana interest na kufanikisha mambo ya watu maskini. Wao hawapendi wamaskini wala umaskini wao. Huyu mama hana muda wa kuwenda ubungeni kwa viti maalamu kuwatetea maskini. Anajijua na wao kama familia wana yao. Kiukweli Chadema ilikuwa ngazi tu ya kutumiwa kupata sifa umarufu short lived.
ReplyDeleteMungu yupo. Atawalinda Watanzania na watu wake.
HIVI WATU MNAOHOJI MAAMUZI YA HUYU MAMA MNAANGALIA PANDE ZOTE AU MNAFIKIRIA UPANDE MMOJA? NILITEGEMEA MNGESEMA KUWA AMEFANYA MAAMUZI YA BUSARA PIA KWA KUKATAA NAFASI AMBAYO INGEENDEKEZA UFALME WA WATU KUPEANA MADARAKA KWA UDUGU, BABA, MAMA, NA WATOTO?
ReplyDelete