Wednesday, November 11, 2015

RAIS KENYATTA AAGIZA WALIMU KULIPWA MISHAHARA YAO YA MWEZI SEPTEMBA

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza walimu nchini humo kulipwa mishahara yao ya mwezi Septemba, na kuitaka Tume ya Huduma za Walimu (TSC) pamoja na vyama vya walimu kujadiliana juu ya ongezeko la mshahara.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano uliofanyika Ikulu ukihusisha makamishna wa TSC pamoja na maafisa wa Chama cha Taifa cha Walimu Kenya (Knut) na kuafikiana kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa malipo ya walimu.

Rais Uhuru ameziagiza pande zote hizo kufanya mazungumzo ndani ya mwezi mmoja, ili kufikiwa makubaliano yatakayoweza kuafikiwa na kutekelezwa na pande zote.

1 comment:

  1. Inapofikia kuhusu maswala ya waalimu lazima kuna tatizo la kupunjwa au kutokulipwa mishahara! Ni jambo lililoko kila kona ya nchi za Afrika. Mbona watumishi wengine wao wanalipwa mishahara tena mizuri!! Hawa ndio wanaowafundisha wataalamu wengi na hata wanaokuja kuingia serikalini hadi mawaziri iweje wanafanyiwa vitendo vibovu!
    Ukienda Uganda, Tanzania Msumbiji utakuta yote hayohayo!!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake