ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 6, 2015

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HAZINA

Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika makao makuu ya Wizara ya Fedha(HAZINA) kwa ziara ya kushtukiza leo mchana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Servacius Likwelile.Rais Magufuli alitembelea na kukagua ofisi zote wizarani hapo na kisha kuongea na viongozi waandamizi.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Fedha ambao ni walemavu Bwana Fundi Maruma na Frank Mkyama wakati Rais alipofanya ziara ya kushtukiza wizarani hapo leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo ambapo alitoa maagizo ya kuziba mianya ya wakwepa kodi.(picha na Freddy Maro)

13 comments:

Anonymous said...

Aina hii ya utendaji kazi imepitwa na wakati, ni ya kizamani mno haendani na mzingira ya leo. Kumkuta mtu yupo ofisini haina maana kwamba huyo mtu anafanya kazi vizuri. Hivi kwa ukubwa wa Tanzania Rais utatembelea ofisi ngapi wewe binafsi na kusimamia watu wafanye kazi! Cha Msingi nadhani ni kuweka mfumo mzuri wa kisasa ambao unakuwezesha kusimamia utendaji kazi kwa kuweka malengo na viashilia ua vigezo vya kubainisha ufanikishaji wake, ambavyo vitaenda sambamba na kuzawadiwa (earnings) au kuwajibishwa (penalties). Ndiyo maana kuna watu wanasema labda alienda kuangalia hazina imebaki na kiasi gani baada ya matumizi makubwa ya kampeni na sherehe za kushangilia ushindi na kuapishwa Rais mpya ambapo watu waliserebuka mpaka asubuhi. Hivi baada ya mapumziko na sherehe hizi, ulitarajia kuwakuta watu wangapi maofisini! Kazi tuuuuuuuuu.. Wikiendi njema.

Anonymous said...

THIS IS JUST ANOTHER PHOTO-UP OPPORTUNITY..... NOTHING MORE NOTHING LESS. ORDINARY TANZANIANA SHOULD BRACE FOR ANOTHER TOUGH FIVE YEARS UNTIL THE OPPORTUNITY COMES FOR THE BIG SHOTS TO GO ACROSS THE COUNTRY AND ASK FOR THEIR VOTES, AND MAYBE FOR THE WANAINCHI TO GET "SOMETHING SMALL" FROM THE CANDIDATES!!!

Anonymous said...

Watanzania ni watu wa ajabu sana,hamna lililo na heri.mkipewa mbivu - ooh imeiva sana, je,mbichi- ooh mbichi sana hailiku.
We become so negative in everything. ..

Anonymous said...

Negativity is the mother of failure; never a mother of success!

Anonymous said...

There's no such thing as "mfumo wa kisasa" utakaofanikiwa bila ya kuwa na kiongozi ambaye yuko tayari kufuatilia! Russians say, "doveryai no proveryai", meaning "trust but verify", a proverb that was adopted and frequently used by former U.S. President Reagan (RIP).

Anonymous said...

Kazi Tu na Dawa, Msemo mpya huo. Nchi hii ina sikukuu nyiiingi za mapumziko utafikiri iko katika "the top ten" kwa maendeleo. Starehe nyingi zinahitaji pesa na kama huna pesa lazima kufanya "mishe mishe" na huo ndio mwendo wa mbele kwa mbele. Kazi kwenu wapiga maboksi huko majuu... mtajiju!!!

Anonymous said...

nyinyi anonymous wa 11:08am na 11:16am, labda hamjui jinsi wafanyakazi hasa wa serikali wanavyofanya kazi!!! alichokifanya rais ni sahihi kabisa, wizara ya fedha watu hawafanyi kazi. wewe kilaza tea break gani mpaka saa sita mchana. wote hao pamoja na boss wao wameshapewa tea break forever. hapa kazi tu## hatuhamishi watu tunafukuza. tulisema itakuwa serikali ya mchakamchaka na ndio huvyo sasa. ukizembea kazini jembe linakupitia. utawajua ukawa mlitaka mmeanze kupiga deal, sasa kibokoo yenu huyo na ulizi tumeshaubadilisha hauhujumiwi mtu hapa.

Unknown said...
This comment has been removed by the author.
Unknown said...

Safi sana tinga tinga hapa kazi tu. Hapa kazi tu hakuna kulala. Nasema hakuna mpuuzi hapa atakaeweza kumfundisha kazi magufuli. Anauhakika na anachokifanya kwa hivyo tunaomba yatieni kufuli madomo yenu mabovu.Mr Magufuli is more than twenty years working experience with the PHD educational level he exactly knows what he's doing. Isipokuwa sisi watanzania na hasa chadema ni watu wa hovyo hakuna kizuri atakachokifanya magufuli mkafurahia kwa sababu nyinyi ni wanafiki. Kama nyinyi mnasema staili hiyo yakwenda kutembelea kwa kushtukiza imepitwa na wakati unafikri Lowasa angeweza angalau kunyanyuka kwenye kiti chake? Lowasa ingemchukia si chini ya mwezi mmoja kufikiria nini afanye . Kwanza kabisa licha ya Mueshimiwa Raisi kufanya ziara ya kushtukiza katika kuanza kuzikagua wizara za serikali vile vile amekwenda kujitambulisha. Ahsante sana tinga tinga waonyeshe mawaziri wako utakao wachagua jinsi gani kazi zinatakiwa kufuatiliwa sio kukaa officini na kusubiri kuletewa dropout. Mungu ibariki Tanzania.

Anonymous said...

Okay now..nyie Chadema grow up! Kama mnamlaumu Rais kufanya kazi yake, mnataka afanye nini? Jee? huyo fisadi wenu EL atawatembelea akina nani besides Ranchi zake za ng'ombe kule Monduli? Tunajua how depressed you are.. we feel your pain of loosing an election. Be reminded that, there is life after a devastating loss..acheni wazimu wenu and GET A LIFE LOSERS!

Anonymous said...

Wewe unayejiita Sallen Marlon (fake name) wewe ndio mfano mzuri wa kuitwa kibaraka wa ccm. You are proving using ccm's system of hatred, bullying and anger to intimidate others just because they are from the opposite side with different point of views. About 99.9% of ideas from ccm followers are filled with anger, hate, intimidation, and bullying even if they are educated. They can't discuss issues civilly even when you agree or disagree. Hiyo ndiyo shida. And this is a big problem when ccm and its followers come in by using peace in the country for their advantage to rule by power of force something which in not fair. Let us all be civil even when we disagree with one another.

Anonymous said...

Hata Lowasa alifanya ziara ya kushtukiza pale alipowatembelea bodax2, mama ntilie wa Temeke..

Unknown said...

Marlon.
We mdau wa chadema unaelalamika kuhusu Sallen Marlon kutoa maoni yake zaidi kuegenea CCM ungemaindi your business first. Nyinyi watu wa chadema uzushi na uwongo ni maisha yenu ya kila siku kwa hivyo jirekebisheni na hiyo tabia yenu chafu kabla hamjaanza kukosoa wengine. Tena naomba kuwa muangalifu na kakuli yako ya kumuambia mtu jina lake fake wakati huna uhakika na unachokisema na huo ndio uzushi wenyewe unaouzungumzwa na watu, chadema muuwache. Unalalamikia mtu anajina fake kwani wewe hilo jina la" Anonymous" ni jina lako halisi? Nyinyi wa chadema mmejaa katika mitandao kazi kutoa taarifa za uongo na chuki na za kupotisha kwa Serikali na viongozi wake, Serikali sawa lakini ile nchi ni yetu sote achilia mbali serikali ya CCM. Kuna mambo mazuri mengi tu serikali ya CCM imeyafanya na wanaendelea kuyafanya ambayo yanapaswa kupongezwa. Moja ya jambo ambalo CCM wanapaswa kupongezwa ni hili la kumuengua Eduwadi lowasa kugombea uraisi kwa ticket ya chama chao. CCM walimuengua lowasa huku wakiwa na uhakika ya kutokea machafuko ndani ya chama chao lakini kwa uhakika kabisa waliona maslahi ya Taifa kwanza chama baadae. Badala yake nyinyi chadema baada ya kwenda mbele mkarudi nyuma kwa kuchukua makapi ya CCM baada ya kuweka maslahi ya Taifa kwanza mkaweka ya chama chenu kwanza kwa kumchukua lowasa kwa kuamini atakisadia chama chenu sio Tanzania sasa kwanini watanzania wasikuazibuni kwa ulaghai wenu? Kwa hivyo kila mtanzania anahaki ya kujibu kila hoja za uwongo zinazolenga kuupotosha umma tena ikiwezekana kwa guvu zake zote. Kwa mfano kila mtu au mtanzania anafahamu uzalendo uliotukuka wa Dk magufuli na nia yake wa kujitoa wote kulitumikia taifa sasa wanatokezea wapuuzi wanaanza kubeza jitihahada zake halafu mnategemea watu wakae kimya bila ya kujibu? Hilo la kukaa kimya halitatokea. Kwanza kabisa watu wa chadema si watu wenye kuweza kujenga hoja za msingi katika mazungomzo mara mnakasirika, matusi mara tu mnapozidiwa hoja anyway tangu lini hoja za uongo zikawa na nguvu? Kwa hivyo tunasema kusoma sio kuelimika kwani kuna watu wa chadema wanajiita wasomi na katika kutaka kuwathibitisha watu kuwa wao ni wasomi wanajaribu hata kikisusia kiswahili katika mazungumzo yao anyway tunajua wote ni ulimbukeni la msingi ni jinsi gani chadema wanatakiwa kuelimika na ni hili la kuendelea kujitoa fahamu ya kutokukubaliana na matokeo ya uchaguzi wakati hata marekani amepekeka salamu zake za pongezi kwa serikali ya Tanzania hii ina maana ya kwamba ukawa,/chadema na lowasa wanaendelea kutekeseka na uchaguzi watu wanasonga mbele na wataseka sana labda wabalike.