ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 5, 2015

Rasmi Dr John Pombe Magufuli, ni Rais wa awamu ya Tano Tanzania. Nini maoni yako katika hili?


Rasmi Dr John Pombe Magufuli, ni Rais wa awamu ya Tano Tanzania.

Nini maoni yako katika hili?

11 comments:

Anonymous said...

haya maoni yanayotakiwa au kuchangia yanasaidia nini ewakati ni Rais tayari na ana maamuzi yote. sisi tutamuamulia au tumpe maoni gani! tuacheni tuendelee na mlo mmoja hadi hapo mungu atakapotuona vinginevyo. umesikia kabisa akiapa atalinda katiba na ilani! Tanatarajia timu mpya isukwe sivyo tutaendelea kuimba nyimbo ile ile.. viva JPM....

Unknown said...

Tumshukuru Mungu nchi yetu haikuingia kwenye vurugu na upotevu wa amani katika kipindi hiki cha uchaguzi. Ilikuwa chupuchupu (almanusra) tu watu hawakuchinjana. Tusirudie tena hii kitu. Ni rahisi sana kupoteza amani na ikishapotea kuirudisha ni vigumu sana.

Nilimpigia debe Mh. Magufuli na nimefurahi amechaguliwa. Lakini hii haitoshi kwa Tanzania. Maendeleo ya kweli yanahitaji kuwepo na upinzani wenye nguvu ili kuisimamia serikali ipaswavyo.

Ni muhimu upinzani (hasa UKAWA) wamalize matatizo yao ya ndani (ndio matatizo yapo) haraka halafu waibuke upya, wakishirikiana na vyama vingine vya upinzani kuisimamia serikali kwa manufaa ya sisi wananchi wote (wapenda CCM na wapenda vyama vya upinzani).

Nina imani na Mh. Magufuli lakini umma wa waTanzania unawategemea sana upinzani (kama viranja) kuhakikisha maendeleo yanakuja Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania.

Anonymous said...

nikupongeze ndg Dr. JPM kwa kuibuka na nafasi hiyo kubwa jappokuwa kwa utata ulioifumbika Tanzania na wapiga kura. Umewshakuwa Rais wa waTANZANIA. Kama utakubali kuendelea kukumbatia katiba ya kizamani na kuitupilia mbali ile yenye mapendekezo ya wananchi basi linalofuata hapo tunakuomba ushirikiane na msajili wa vyama kufuta kabisa mfumo wa vyama vingi nchini kwani hauna umuhimu kwani ni kupoteza fedha za walipa kodi na wapiga kura wanapoteza muda wao bure kura zao hazihesabiwi kabisa! mahesabu yanayotolewa ni yalle waliyojipangia wenyewe tume. Hatujijui ni lini Tanzania itakuwa na Demokrasia halali. Pili kama utaendelea na timu ya kuambiwa mweke huyu basi ujue tayari unaharibu mwelekeo wa yale uliyotuahidi NEEMA. Tunatarajia kuwa na umeme na maji tosha uwezo upo na pia mishahara iliyookosekana kwa matumizi ya kampeni wafanyakazi warejeshewe haraka hasa waalimu.

Anonymous said...

ASANTE DR. JPM skwa kupata nafasi ya kuwatumikia waTanzania. Ulisema mengi sana kwenye kampeni zako moja kubwa kikiwa kufufua viwanda na ukiwa mkoani Kilimanjaro ulisema nanukuu "Nataka wenye viwanda Moshi vianze kufanya kazi wiki mbili zilizobakia kuendea uchaguzi mkuu" mwisho. Nivyema ukajitahidi kuanda timu itakayotekeleza. WATanznaia tunaishi maisha ya ajabu na sijui kama unaliona hilo ukishaingia pale penye neema mara nyingi unasahau na ndicho tunachokiangalia. Mafisadi wote unao humo ndani wamekunja makucha yaoo, je unawachukuliaje? Bunge lako lisiwe la makelele kama yaliyoopita na mbunge yeyoopte atakayelala bungeni tunaomba aondolewe mara moja bila kusita. Waziti yeyote atakayekosa kutekeleza wajibu wake usimbadilishe wizara kwani hali hii imeendelea kulimaliza taifa. kila heri. tunakutizamia.

Anonymous said...

Uchaguzi umekwisha,watu waondoe tofauti zao za kisiasa ,tuelekeze nguvu zetu katika kujenga taifa.

Anonymous said...

Maoni yangu ni Tanzania chini ya utawala wa CCM itaendelea kua nchi maskini

Anonymous said...

Bora kuwa maskini chini ya muadilifu kuliko kuishi katika ufukara ambao ungesababishwa na genge la mafisadi na wahuni wa UKAWA!

Anonymous said...

maoni ni ujinga mtupu..raisi wa muungano upi wakati znz mpaka sasa hakieleweki....yani ujinga na ndiyo maana nchi kama Rwanda sasa inatuzidi na wataendelea kwani sisi sijui tunaenda wapi...mtakao pinga jiangalieni kama mtakuwa na maisha bora in 2 yrs wewe na ndugu zako

Anonymous said...

Tanzania itaendelea kuongozwa na ccm na itaendelea kuwa MASKINI, mpaka hapo wananchi watakapoamua kuamka maana bado wamelala kwa kupewa dawa ya usingizi na ccm

Unknown said...

Maoni yangu ni kwa upizani na wanaoshabikia upizani kwa kuamini kuwa mabadiliko hayawzi kupatikana isipokuwa kwa viongozi wa upizani hizo ni fikra mgando na duni. Mifano ipo mingi katika nchi nyingi ambapo viongozi wa upizani pamoja na wanaowashibikia kwamba wangeweza kuleta mabadiliko ya kweli kuliko serikali au vyama vinavyoongoza serikali husika lakini baada ya wapizani hao kupata nafasi kushika hatamu za kuziongoza serikali hizo kilichotekea ni uozo mtupu wa uongozi kutoka kwa upizani. Mfano mzuri sana ni Marekani ni taifa lililoendelea kwa kila nyanja sisi watanzania tungetamani nchi yetu iwe lakini wakati wa Bill Clinton wakati yupo madarakani Republican walikuwa wakimsemea ovyo sana yeye na chama chake cha Democrat kwamba nchi ilikuwa ikiendeshwa hovyo sana chini ya utawala wao na imepoteza hadhi ya marekani. Republican waliapa kwamba watafanya kila wawezalo kuirejeshea marekani heshima inayostahili pindi tu wakishinda uchaguzi. Mungu bariki uchaguzi ukafanyika na Republican chini ya uongozi wa George Bush wakashinda uchaguzi kilichotekea chini ya uongozi wa George Bush kwa marekani sidhani kama nina haja ya kuelezea kwa sababu kila mtu anajua sio wa Marekani tu bali dunia zima. Na wamerekani nadhani walijifunza kitu baada ya kilichotekea kwa Republican chini ya uongozi wa George Bush hadi kuja kumchagua Obama. Licha ya maneno mengi yanayosemwa na wapinzani kuhusu utendaji wa kazi wa Obama. lakini Obama kwa kiasi fulani ametimiza ahadi yake alioiyahidi ambapo wakati wa kampeni aliifananisha Marekani na hali ya uchumi wake sawa na Gari liloingia msingini na kukwama kwa hivyo Obama kitu kwanza alichoahidi ni kuja kulikwamua Gari hilo na kulieka barabarani na kwa kweli amefanikiwa sio kulieka gari hilo barabarani tu bali kafanikiwa kulitembeza kwa mwendo wa kasi. Tukirudi kwenye mada yetu nini maoni baada ya magufuli kuwa raisi ni kwa upande wa upizani kama wanaelewa hakuna kitu kitakachobadlisha matokeo ya uchaguzi kwanini waendelee na kupinga matokeo hayo? Na kama idadi kubwa ya wanachi wameridhishwa na kiongozi aliechaguliwa kwanini watu wa upizani wanaendelea kuwashawishi wananchi kutofanya hivyo nini maana yake wanajaribu kuwaamulia wananchi kiongozi gani awaongoze je sasa hii ni haki? Kwa kiasi fulani kutokukubali matokeo kwa upande wa upizani inaonyesha jinsi gani walivyo na uchanga kabisa ya uweledi wa demokrasia na ni haki kabisa kwa wao kutokupata nafasi ya kuiongoza nchi kwani hata kama kutokana na madai yao kwamba wamedhidiwa ujanja na CCM na kuibiwa kura zao basi huu ni ushahidi tosha ya kwamba watu wa upinnzani ni wazembe na ni sio watu makini wamelala mpaka CCM inawaibia kura zao wao wenyewe wapo wapi? Kama wapinzani wanaibiwa kura wakiwa macho wazi vipi tukiwapa nchi watakuwa na uwezo gani wa kuwazuia tembo wasiibwe, watakuwa na uwezo gani ya kuwadhibiti mafisadi wakati wameshindwa kudhibiti kura zao zisiibiwe? --kwa kifupi ukiangalia kwa undani watu wa upizani licha ya makelele mengi ya kutaka kuongoza nchi lakini bado kabisa wanahitaji mtaji mzuri zaidi wa viongozi wenye sifa kwani kwa kumtegemea lowasa pekee, CCM wana akina lowasa au bora kuliko lowasa wengi tu ukilinganisha na upinzani. La kufanya kwa upande wa upizani ni kuachana na msimamo wa kutoyatambua matokeo isipokuwa waanze na mikakati ya kweli ya kuimarisha upizani kwa chaguzi zijazo.

Anonymous said...

Hongera mheshimiwa Rais Magufuli. Ninayo imani kubwa utabarikiwa kufanya kazi nzuri. Utapata pressures from so many distractors, left and right, but stay focused Mr. President to what is good for the country. Huwezi kumridhisha kila Mtanzania, lakini kwako KAZI TUU. Nchi yetu imetoka mbali, na sisi wenye busara tunajua maendeleo hayatapatikana overnight; and as long as we stay the course, Tanzania itasonga mbele. Umoja ni Nguvu wadau, tushirikiane na Rais wetu mpya wa Tanzania..hii ni nchi ya CCM, CHADEMA, ACT, NCCR, TLP, CUF, n.k. We are in one boat and thus, we shall sail together.