Saturday, November 7, 2015

Serikali yasitisha matumizi picha ya Dk Magufuli



Rais John Pombe Magufuli.
By Ephrahim Bahemu, Mwananchi
Dar es Salaam. Serikali imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli ambayo yalitakuwa kuanza leo kwa ofisi zake.
Uamuzi huo ulitolewa jana muda mfupi baada ya Serikali kuzindua picha hiyo, siku tatu tangu Magufuli kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma na wananchi kwa ujumla kwamba imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Joseph Pombe Magufuli mpaka hapo itakapotangazwa tena,” ilisomeka taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari (Maelezo).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, awali majira ya saa 6. 00 mchana jana, Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi ya picha hiyo ambayo ingeuzwa kwa Sh 15,000.
Serikali ilisema itazitangazia ofisi hizo na Watanzania kuhusu kuanza tena kwa matumizi ya picha hiyo.
Uamuzi huo wa Serikali ulitolewa muda mfu baada ya kuzindua rasmi picha hiyo.
Awali Mkurugenzi wa Maelezo, Assah Mwambene alisema jana kuwa picha hizo zipo za kutosha na zinapatikana wakati wowote ilimradi iwe siku na muda wa kazi.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake