
Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuchukua fomu za kuwania uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akizungumza na Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Karagwe Gosbert Blandes akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib

George Nangale akipitia fomu ya kuwania nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kukabidhiwa na Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib katika ofisi ndogo za CCM Lumumba.
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib katika ofisi ndogo za CCM Lumumba.

Banda Sonoko akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib akimkabidhi fomu Ndugu Simon G. Rubugu.
Hawa ndio waliojitokeza mpaka sasa kuchukua fomu Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba ;Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, aliyekuwa
mbunge wa Karagwe,Gosbert Blandes,Leonce Mulenda, George Nangale na Profesa Costa Mahalu, Muzamil Kalokola, Banda Sonoko,Simon Rubugu.
Mungu wangu utusaidie waTanzania. Mh. Sita umeharibu sana utaratibu mzima wa maoni ya katiba yaani tutashangaa sana kusikia unaitaka tena nafasi kubwa hivyo! Yaani nasema kabisa hutatufaa ni vyema ukapumzike kabisa achana na hii siasa kwani umeyumbisha sana mambo. Rais dr JPM bunge litakuwa la kichekesho na fujo kama kweli tutakuwa na kiongozi kama huyu. KAZI TU!!
ReplyDeleteNakuunga mkono mdau wa 3:28PM. Hawa Wanasiasa wakongwe wananishangaza. Wanayo ile mentality ya "ownership" na kwamba ndiyo wao pekee wenye uwezo wa kutekeleza majukumu ya kisiasa na kiserikali. Hii old boys mentality, lazima ikomeshwe, na tuwape nafasi younger politicians. Mheshimiwa Mzee Sitta, tunakushukuru kwa mchango wako wa miaka mingi nchini, lakini wakati wa kujinyakua umefika.
ReplyDelete