
Watu 128 wameuawa katika matukio sita tofauti ya ugaidi yaliyopangwa na magidi jijini Paris nchini Ufaransa.

Katika matukio hayo magaidi 8 wameuawa, 7 kati yao wakiwa waliojilipua kwa mabomu ya kijitoa mhanga.

Magaidi hao pia wamefanya mashambulio hayo katika uwanja wa mpira wa miguu wa Stade de France uliokuwa na watazamaji 80,000 waliokuwa wakifuatilia mchezo kati ya Ufaransa na Ujerumani, na shambulio lingine limefanyika ukumbi wa starehe kulikokuwa na tamasha la Rock .

Kufuatia mashambulio hayo, majengo yote ya umma yamefungwa jijini Paris, shule pamoja na usafiri wa umma pia umesitishwa.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amaetangaza hali ya hatari, na baadhi ya mipaka ya wilaya imefungwa. Viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wameahidi kuisaidia Ufaransa kukabiliana na ugaidi.





No comments:
Post a Comment