Advertisements

Friday, November 20, 2015

WAZANZIBARI WANAOISHI UINGEREZA WAANDAMANA WAKITAKA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD ATANGAZWE MSHINDI WA KITI CHA URAIS

Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza jana walifanya maandamano wakidai haki ya kutangazwa ushindi wa Chama Cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Octoba 25 mwaka huu
Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association (ZAWA) ambapo wazanzibari hao walitoka maeneo mbali mbali katika miji yao na kukusanyika katika eneon la Downing Street kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na uongozi huo kukabidhi barua yao yenye malalamiko kutaka suala la Zanzibar lishughulikiwe.
Maandamano hayo yalifanyika kwa lengo la kuongeza shindikizo kwa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua za haraka ya kuhakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inakamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Zanzibar iliingia katika mkwamo wa kisiasa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha Octoba 28 kutangaza kuufuta uchaguzi wote kwa madai kwamba ulikumbwa na matatizo mbali mbali.
Wakati jecha akitoa tangazo la kufuta matokeo bila ya kushauriana na tume yake alikuwa tayari ameshatangaza matokeo ya kura za urais za majimbo 31 kati ya 54 ya Zanzibar pia washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani katika majimbo hayo walishatangazwa na walishakabidhiwa vyeti vyao.


Rashid Ali ambaye ni kiongozi wa ZAWA alisema jana kuwa wamewasilishwa barua hiyo wakiamini kwamba suala la Zanzibar litashughulikiwa ili wananchi wa Zanzibar waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.


Mwakilishi wa ZAWA, Hassan Khamis alisema wameamua kupeleka barua kwenye ofisi za waziri Mkuu wakiamini suala hilo litashughulikiwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti na za haraka kaika kushughulikia suala hilo ambalo limewaweka wazanzibari roho juu.
Paparazi blog

3 comments:

Anonymous said...

Hamkupiga kura, and so you have no right to protest in a Foreign land. Kwa nini msirudi Zanzibar kufanya hiyo protest yenu. Nyie ni vibaraka wa kutumwa na huyo Maalim wenu, sijui mmelipwa pesa ngapi kufanya hivyo? Uingereza haiwezi kuwasaidia na haiwezi kuingilia siasa ya ndani ya nchi. Zanzibar haipo chini ya ukoloni wa mwingereza, hamlijui hilo?

Anonymous said...

Walioko Zanzibar wako tulii,nyie mnajisumbua na winter hii mmeshika mabango.Hakuna hata mmoja wenu anaejua kile Maalim Seif na Dr. Shein walichoongea na kukubaliana .

Anonymous said...

Watu wa nje hamtoagi misaaada ya aina yoyote ile kuchangia maendeleo nyumbani Ila mnapenda kupayuka na kujidai mnajua kumbe hakuna kitu! Na je, mlipiga kuraa Ama? Kama hukupiga kura kumchagua Shein au Seif baasi you have no right to protest at all.... Asanteeeeni!!!