ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 20, 2015

ZADIA KUFANYA MAANDAMANO IKULU YA MAREKANI KESHO JUMAMOSI

Ndugu Wanachama wa ZADIA
Kufuatia maoni ya Wanachama ya kutaka tuitishe mkutano kujadili hali ya kisiasa huko nyumbani Zanzibar, Uongozi wa ZADIA ulikutana na kujadili swala hilo na kufikia maamuzi yafuatayo:
1- Tuandike barua ambayo itatumwa kwa Wajumbe wa Senenti na Baraza la Wawakili la Marekani. Na kila mwenye nafasi awasiliane na Mjumbe wa Seneti na Baraza la Wawakilishi katika eneo analoishi, kumtaka ashiriki kwa njia moja au nyengine kusaidia kukwamua mkwamo wa Kisiasa Zanzibar.
2-Tufanye maandamano Ikulu ya Marekani (White House) tukibeba mabango na Tamko rasmi la ZADIA kuhusu hali halisi ilivyo Zanzibar.
Kwa hivyo, Uongozi wa ZADIA unawaomba kuhudhuria kwenye maandamano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi, tarehe 21/11/2015.
Tutaanza shughuli yetu saa sita mchana kwa majira ya Marekani ya Mashariki, mbele ya White House. Maandamano haya pia yatawashirikisha wanamabadiliko wote kutoka nchini Tanzania na wapenda amani na Demokrasia  kote ulimwenguni.
Wito unatolewa kujitokeza kwa wingi na kwa wakati. Tafadhali ukiipata taarifa hii mfikishie mwenzako.
Zanzibar kwanza.
Uongozi wa ZADIA.

3 comments:

Anonymous said...

Acheni ujinga,mnatafuta umaarufu

Anonymous said...

Msiwe wapumbafu nyie, la maana ni kuendelea kujijengea maisha bora na kuzitunza familia zenu hapa marekani. Acheni mambo ya siasa kwani, kamwe hamuwezi kubadili hali ya nyumbani kutoka huku ughaibuni. Mkitaka mrudi Zanzibar kufanya hivyo. Hapa mtakalofanikiwa ni kupiga propaganda na kuweka nyuso zenu kwenye local TV stations tuu, and then what? Wamarekani wanayo mambo ya muhimu zaidi ya kuwasikiliza ninyi. Basically, it a waste of your time and resources. Labda mngefanya kule seattle, au baridi ni nyingi kuwa outdoors?

Anonymous said...

Walioko Zanzibar hawana mpango wa kuandamana nyie mnajitoa kutafuta umaarufu usio na tija.