Saturday, December 5, 2015

BALOZI WILSON MASILINGI AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VYAMA VYA SIASA, AHUDHURIA MKUTANO WA HALMASHAURI YA CCM DMV

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi leo Jumamosi Desemba 5, 2015 alihudhuria mkutano wa Halmashauri ya CCM tawi la DMV ikiwa ni moja ya ziara zake anazotarajiwa kuzifanya kutembelea matawi ya vyama vya siasa nchiMarekani yenye lengo la kudumisha mshikamano na ushirikiano wa Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.

Akiongea kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV Mhe. Wilson Masilingi amesema lengo kuu ni kuwa karibu na vyama vya siasa kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano ndani ya Jumuiya za Watanzania nchini Marekani na pia kuvitambua kama sehemu na sura ya Diaspora na kutoa wito kwa Watanzania waishio Marekani kuelekeza nguvu katika kuwekeza nyumbani bila kujali ufuasi wa chama unachoamini au kushabikia, wote ni Watanzania.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliiomba Halmashauri hiyo ya CCM DMV kusaidia katika maendeleo ya Tanzania kwa kupanua wigo wao pamoja na kwamba lengo lao ni siasa na siasa ni sehemu ya maisha ya jamii na maendeleo ya jamii yanategemea siasa, kwa hiyo basi mnaposikia kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza Tanzania msisite Ubalozi upo wazi na utafanya kila liwezekanalo kuhakikisha muwekezaji huyo hapati vikwazo vyovyote.

Mwisho Balozi Wilson Masilingi aliwashukuru Watanzania kwa kuwa mabalozi wazuri nchini Marekani na kuwaasa kuishi kwa kufuata misingi na sheria za nchi ya Marekani.

 Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea jambo na mwenyekiti wa tawi CCM DMV Bwn. George Sebo kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 mkutano uliofanyika Hampton Inn, College Park, Maryland. Picha na Kwanza Production/Vijimambo Blog
Mkutano ulianza kwa sala na kuwakumbuka wote waliotangulia mbele ya haki.

Mwenyekiti tawi la CCM DMV Bwn. George Sebo akifungua kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV

Picha ya pamoja.
Bwn. John Mbatta katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Given  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Catherine  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Aunty Grace Sebo  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Grace Mlingi  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Mzee Joel  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Dr. Secelela Malecela  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Katibu wa CCM DMV Bi.Jesca Mushala  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Mwenyekiti wa CCM DMV Bwn. George Sebo  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.

7 comments:

Anonymous said...

Wana DMV pamoja na balozi wetu. Hebu tukaeni chini tuwe na mawazo endelevu! huu mtindo wa matawi ya CCM hapa ughaibuni yanatusaidia nini, na je hivi ni kazi ya BAlozi anayeiwakilisha nchi!! Wana DMV badala ya kukaa kuelekeza nguvu zetu kwenye kutafakari yale muhimu kama kuandaa rasimu ya ile Uraia pacha ili marekebisho ya katiba inayookuja tuombe iingie mle! tunakaa vikao vya matawi ya vyama na wakati hatutapig kura tukiwa huku ughaibuni na isitoshe wanachama ni wachache kuliko idadi ya wanaoomba uraia pacha upate Baraka! wadau na wana DMV, Mh. Balozi hebu tuwe na mwelekeo wenye tija na manufaa.. Asante.

Anonymous said...

Magufuli futa futa haya matawi ya vyama ughaibuni
Ibakie tu chama cha Watanzania Kila inchi
Hivi nchi gani duniani ina vyama ktk nchi nyinyine
Unatuletea ugombanishi huku ughaibuni sasa hivi
Hatuwi Watanzania Bali tu wanasiasa
Vijembe, kuchomeana, umbea kama kina nape na Makonda
Pls Magufuli futa vyama vyote ughaibuni

Anonymous said...

Ndo hawa hawa wasiolipa kodi wakileta makonteana Tanzania

Anonymous said...

Heko kwa maoni yote hapo juu. Jamani wote huku tunajiita tumetokea Tanzania na kamwe husikii mimi ni CCM au UKAWA wa kutoka Tanzania. Huo sio ustaarabu kabisa. Mbona hata husikii kwa zaidi tukisema mimi mchaga au mmakonde au mhaya au mmasai kutoka Tanzania. Haya yote tuyaache na tuanzie kwa hawa viongozi wanaotoka huko nyumbani Tanzania. Tuache matabaka ya kichama, kidini na ukabila. Tuwe na umoja wa Watanzania that's it hapo ndio ustaarabu. Kama mdau wa kwanza hapo juu alipotoa oni lake la kupatiwa uraia Pacha au Dual Citizenship, hiyo ndio swala la msingi na muhimu sana wakati huu. Na kwa niaba ya Wana diaspora wote wa Watanzania popote walipo hapa Duniani, tunaiomba serikali ya Rais John Pombe Magufuli ilishughulikie hili swala at least katika kipindi chake cha miaka mitano or less hili swala lipitishwe na kuwepo na uhalali wa Dual Citizenship. It can be done!! Hii ikitokea, Tanzania itaweza kuwa na maendeleo makubwa kwa pande zote kiuchumi, kielimu na hata kiafya na zaidi. Again, it can be done!!

Anonymous said...

Angalieni utendaji wa ofisi kuhusu masuala muhimu kuliko kuanza kutembelea Matawi maana uchaguzi umeshapita.
Rekebisha yafuatayo;

1. Utendaji kazi wa watumishi hapo ubalozini
2. Ustaarbu wanapojibu simu maana hiyo ni ofisi ya serikali sio ya mtu binafsi
3. Ukielekezwa kwenye extension Yeyote zinakuwa zimejaa huwezi kuacha maagizo.
Tuanze na haya kwa sasa maana utendaji bora unahitajika.
HAPA KAZI TUU.

Anonymous said...

Haya matawi yaliyoibuka ughaibuni ni kwa mkono wa uongozi uliokuwepo madarakani na nadahni umetumia fedha nyingi sana kuruhusu kada kutembea state kibao kufungua matawi hivi ni wapi tutakapotundika au kupandisha bendera ya CCM AU TLP, CDM AU NCCR huku ughaibuni kama sio ndoto za alinacha?? Tunashindwa hata kuchangia kusaidia baadhi ya maeneo Fulani kule nyumbani. Hebu Mh. Balozi tusiendeleze haya matawi ni vyema yafutike kabisa kwani unis ya uchonganishi na wala sio ya kujenga jamii ya waTanzania..

Anonymous said...

Hivi huyo balozi angeitwa na chama kingine sio ccm angeenda?kwasababu balozi Yuko hapo kuwakilisha watanzania wote.aachane na mambo ya vyama.huo muda si angekaa ofisini na kutatua matatizo hapo ofisini kama mdau wa hapo juu alivyosema.najua hizi msg zitamfikia balozi.kama amekuja kuwakilisha chama au vyama vya siasa basi tuambiwe tujue.Balozi kachemsha kwa hili.najua kuna wafanyakazi wake wanasoma aambie asirudie hizi vitu.