Sunday, December 6, 2015

KWA STAILI HII KIPINDUPINDU KITAENDELEA KUTUTESA SANA

Hali halisi ya makazi ya wananchi wa Uswazi kiwalani BomBom 
Mtaro uliopo kwenye soko la Tandika 
Mtaro wa Soko la Tandika bado ni hatari kwa maisha ya wafanyabiashara na akimama ntilia wapo hapo 
Soko la Tandika 
Hapa kazi mwana bila hivi utahama mji na kupiga chabo 
Mama akiwa na mtoto wake katika soko la Temeke atazoea tuu mazingira lakini jee Afya yake itakuaje hali ya uchafu 
Wafanyabiashara katika soko la Temeke Stereo wakiwa kazini 
Hali ya soko la la Temeke Stereo lilivyoshona 
Soko la Temeke Stereo hali kama hii huku watu wakiokota matunda yaliyotupwa 
Takataka katika soko la Temeke stereo uchafu uliokithiri picha inawaonyesha watu hao ambao wanaokota matunda yaliyotupwa jee kipindupindu hakiwezi kumalizika 
katika maeneo kadhaa katika jiji la Dar es salaam hususani uswahili ni magonjwa ya kipindupindu na magonjwa ya tumbo na kuhara 
Mifereji iliyojengwa ni midogo haiwezi kukizi hali ya mvua kubwa picha hii ni makaazi ya eneo la Buguruni kwa mkanda 
Huu ni mfereji uliojengwa chini ya kiwango katika eneo la Buguruni mnyamani kuwanusuru wakaazi hao ili kuepukana na mafuriko yaliyowakumba mwaka jana sambasamba na viongozi wakuu wa nchi wastaafu kutembelea eneo hilo na kuwa pa matumaini wakaazi hao lakini mvua kidogo mafuriko kama kawa
Hivi ndio hali halisi ya Uswazi katika kufanya usafi wa mazingira siku ya Desemba tisa tukumbuke lazima tuzingatie kutokomeza kipindupindu tuingie uswasi na madawa eneo la Buguruni mnyama 
Hivi ndivyo hali ilivyo ukiona aibu huli hapa kazi tuu kama alivyonaswa na kamera ya mzuka mfanyabiashara wa mbogamboga katika eneo la buguruni mnyamani kandokando ya reli akiwa anatwanga kisamvu kwenye kinu leo

HABARI ZA JAMII

No comments: