Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole, kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wapili kushoto) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke, na kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Robert Tibagwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia) na Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Robert Tibagwa
1 comment:
Mhe Waziri usikubali tena mambo ya kutoa uraia halaiki!
Post a Comment