Sunday, January 10, 2016

BAND YA SKYLIGHT SASA IMEKUJA KIVINGINE NJOOLEO UONE MAMBO MAPYA NDANI YA ESCAPE ONE

Mwimbaji wa Bandi ya Skylight, Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) uku akisindikizwa na Natasha(kulia) pamoja na Leah ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita sasa leo sio siku ya kukosa njoo ujionee mambo mapya kutoka kwenye bandi ya Skylight.
Sam Mapenzi akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Suzy na Sony Masamba kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
Waimbaji wa bendi ya Skylight, Joniko Flower na Sony Masamba wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Bamutu ya Kongo wakisakata rhumba kwa staili ya aina yake Joniko Flower na Sony Masamba wakionesha umahiri wao mbele ya mashabiki.
Mashabiki wakiendelea kusebeneka na burudani ya Skylight Band.
Sam Mapenzi ni muimbaji mashuhuri na huwa anajua kukonga nyoyo za watu hususani katika ule muziki wa Afrika magharibi weee utampenda hata kwa mkopo, hapo akiwa anaimba kwa kushirikiana na Suzy ndani ya bendi ya Skylight.
Mwimbaji wa Bandi ya Skylight Suzy (kulia) akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akisindikizwa na Sony Masamba ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Sam Mapenzi ni muimbaji mashuhuri na huwa anajua kukonga nyoyo za watu hususani katika ule muziki wa Afrika magharibi weee utampenda hata kwa mkopo, hapo akiwa anaimba kwa kushirikiana na wenzake ndani ya bendi ya Skylight.
Sony Masamba akichana mistari kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku Suzy pamoja na Sam Mapenzi wakipiga back vocal.
 Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha sehemu ya mashabiki pamoja na waimbaji wa bendi hiyo ndani ya Jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza‬ kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Waimbaji wa bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni.
Kasongo Junior na Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Kasongo Junior na Suzy wakilisakata rhumba mbele ya mashabiki wao waliofika kuona mambo mapya kutoka katika bendi ya Skylight band.
Leah kutoka Skylight Band akiendelea kuwapa raha mashabiki wake ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jumapili iliyopita ambapo leo pia mwendo ni ule ule, bila kukosa njoo wewe na yule waambie na wengine pia bila kukosa katika fukwe tulivu kabisa.
Mashabiki wakiendelea kuziludi ngoma za Skylight ndani ya kiota cha Escape one jumapili iliyopita.
Mwananziki wa bendi ya Skylight Sony Samba akiimba moja ya sebene la bendi hiyo uku waimbaji wa Skylight wakendelea kuserebuka ndani ya Kiota cha Escape One Mikocheni
Mwimbaji wa Band ya Skylight,  Kasongo Junior akishusha mistari ya kufa mtu mbele ya mashabiki wao waliofika kwenye kiota Cha Escape One huku akisindikizwa na waimbaji wenzake ambao ni Leah, Suzy pamoja na Natasha.
Sony Masamba akichana mistari kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku Joniko Flower, Sam Mapenzi na Kasongo Junior wakimsikindiza kwa miondoko ya aina yake.
 Mwimbaji wa bendi ya skylght Natasha akiwa anawapa mashabiki vionjo vya nyimbo za taratibu (kistaarabu) huku akisindikizwa na Suzy  pamoja na Kasongo Jonior jumapili iliyopita ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni. 
Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha mashabiki wao huku akisindikizwa na waimbaji wa bendi ya Skylight ndani ya Jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza‬ kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Waimbaji wa Bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani katika kiota cha Escape One 
Tofe aka 2be ambaye ni Mpiga Bass akiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wao katika kiota cha Escape One Mikocheni Jumapili iliyopita.




No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake