BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limezidi kutoa wito kwa Waimbaji wa muziki wa Injili kujisajili katika baraza hilo ili stahiki zao zitambulike inavyotakiwa.
Mkurugenzi wa ukuzaji Sanaa na Mtukio wa Basata, Maregesi Kwirujira Ng’oko alisema waimbaji wengi wa muziki wa Injili wa Tanzania kuzingatia hilo.
Ng’oko alisema kujisajili Basata kuna faida na fursa nyingi ambazo ni msaada ambao utasaidia kupata haki zao kupitia kazi zao.
Ng’oko alisema kwa kuwa wao ndio wasimamizi wa kazi za sanaa ni jukumu lao kuwakumbusha mara kwa mara wasanii kujisajili.
Aidha Ng’oko alisema wanatoa salamu hizo kwa wasanii pindi inapotokea mikinzano katika ufanikishaji wa kazi zao.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Abihudi Mang’era alisema wanafikiria kuongeza msukumo kwa waimbaji wa muziki wa Injili kuhusu kujisajili Basata katika baadhi ya matukio.
Mang’era alisema wanafikiria kutoa elimu ya kujisajili Basata katika matamasha yao ama kusaka namna ya kufanikisha utambuzi wa waimbaji katika baraza hilo.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake