Arusha.Mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa nchi ya Burundi yameanza jijini Arusha bila serikali ya nchi hiyo kutuma wawakilishi kwenye mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Ushirikiano wa kimataifa,Dk Augustino Mahiga amesema leo kwenye makao makuu ya EAC kuwa serikali ya Burundi imeomba kikao hicho kusogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali.
Hata hivyo hakua tayari kutaja sababu hizo. Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi za maziwa Makuu(ICGLR)Georges Chicoti,Waziri wa Ulinzi wa Uganda,Crispus Kionga ambaye ni mwakilishi wa mpatanishi wa mgogoro huo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera.
"Mkutano huu ni kuileza dunia kuwa tumejitolea kuhakikisha tunashirikiana na nchi ya Burundi kuelekea kutafuta amani ya mgogoro ulioanza mapema mwaka jana ,"amesema Dk Mahiga
Amesema kutokana na mkutano huo kukosa wawakilishi wa Burundi umesababisha mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokua ufanyike Januari 8,jijini Arusha kusogezwa mbele kwani ndio ungejadili mapendekezo ya mkutano wa leo.
Waziri Mahiga amehaidi kutoa taarifa zaidi baada ya mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake