Wednesday, January 6, 2016

Fastjet kuzindua safari kati ya Tanzania na Kenya

Shirika la ndege la bei nafuu lapanua wigo wa safari zake barani Afrika na kufungua safari ya kimataifa ya moja kwa moja kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam na Kilimanjaro.



 Januari 2016 – fastjet imetangaza safari yake mpya ya kimataifa ya kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi, Kenya kuwa itaanza rasmi mnamo tarehe 11 Januari 2016.

Fastjet imepewa ruhusa na serikali ya Kenya kufanya safari zake nchini humo kufuatia makubaliano ya pamoja na mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya, kama ilivyopitishwa na serikali ya Tanzania.

Vilevile Fastjet imetangaza kuwa inatarajia kuzindua safari zake za anga kati ya Zanzibar na Nairobi na pia kati ya Dar es Salaam na Mombasa ambapo uzinduzi huo utafanyika mapema mwaka huu 2016.

Tiketi za kurudi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwenda uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na uwanja wa ndege wa Kilimanjaro zitakuwa za kila siku mara tu baada ya uzinduzi huo na wasafiri watasafiri na ndege ya kisasa aina ya  Airbus A319 ambayo hubeba abiria 156.

Kwa mujibu wa Fastjet, safari nyingine za ndege zinatarajia kuzinduliwa kufuatia kuongezaka kwa maombi ya wateja wake na hii ni kwa sababu ya unafuu wa bei zake sambamba na huduma bora.

Tiketi za safari hii mpya zimeanza kuuzwa, na nauli za Nairobi/Dar es Salaam zitatozwa kwa $50 kwa safari moja, na Dar es Salaam/ Nairobi zitatozwa kwa $80 kwa safari moja.

Nauli hizi ni pamoja na kodi ya serikali  ambayo itachajiwa. Kwa mantiki hiyo, Fastjet inawaomba abiria na wateja wake kwa ujumla kufanya booking mapema iwezekanavyo ili kufaidika na bei nafuu ambayo hutozwa kuliko ndege zote ambazo husafirisha abiria kati ya nchi hizi mbili.

“Usafiri wa anga katika uwanda wa Afrika mashariki umekuwa na ushindani mkubwa  kutokana na safari nyingi bado hutoza nauli kubwa jambo linalosababisha abiria wengi kushindwa kumudu safari hizo” alisema John Corse, Meneja Mkuu wa fastjet kanda ya Tanzania.

“Wasafiri wengi wanaosafiri kati ya miji hii miwili mikubwa yenye idadi ya watu wasiopungua milioni 8 hapa Afrika Mashariki wamekuwa wakipatwa na vikazo mbalimbali vinavyowarudisha nyuma kutokana na bei ya safari za ndege kuwa kubwa ambayo tunaamini imewakatisha tamaa wasafiri wengi”, alisema Corse.

Matarajio ya Fastjet kufanya safari zake nchini Kenya zitaleta matumaini mara tu baada ya shirika hilo kuzindua safari hizo ambazo bei zake zimepokelewa na wateja wengi wanaosafiri na ndege zingine hasa pale ambapo nauli za Fastjet zimepungua kwa asilimia 40 hivi.

“Jambo kuu la msingi ni kwamba ushindani ni muhimu kwa wateja, kwa kuwa inampa mteja nafasi ya kuchangua unafuu wa nauli atakayoimudu, na hali hii hufanya watalii na wajasiriamali na wageni wanaotembelea nchi hizi mbili kuwa huru kuamua kwa raha kati ya Tanzania na Kenya” Corse alisema.

“Hali hii baadae italeta maendeleo ya pamoja kati ya nchi hizi mbili ambapo ukuwaji wa biashara zao za ndani na nje, vilevile pia utalii utaimarika kwa kiasi kikubwa na itakayo pelekea kukua kwa uchumi wa nchi hizi mbili”, aliongeza Corse.

Pia alisisitiza kuwa haileti maana halisi kwa mgeni ama mtalii kusafiri kwa zaidi ya masaa 12 kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi Kenya na kumfanya achoke kama ilivyo katika safari zingine. Na kwa kuwa sasa Fastjet imezindua safari mpya kama hii ya nchi na nchi, basi inategemea wasafiri wengi watafaidika na huduma za Fastjet.

Kwa kuunga mkono mategemeo haya hapo baadae, hii ni baada ya Fastjet kufanya utafiti wa kina na kubaini kuwa  abiria wake waliweza kumudu bei zao na kuzikubali moja kwa moja.

Safari za kila siku za fastjet kutoka Dar es Salaam zitaanza saa 3:50 asubuhi na kutua Nairobi-Kenya saa 5:10.

Safari za kurudi kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam zitaanza saa 8:10 na kutua saa 10 :05 kulingana na saa za Afrika mashariki.

Safari za kwenda Kilimanjaro kutoka Nairobi zitaanza saa 5:10 na kutua saa 6:40 na safari ya kurudi kutoka Kilimanjaro kwenda Nairobi zitaanza saa 7:10 na kutua saa 8: 40 kulingana na saa za Afrika mashariki.

Fastjet inatoza nauli iliyo nafuu kadri iwezekanavyo na kwa kutozingatia gharama za ushuru wa mizigo, vinywaji lakini vyote hivi vinapatikana kama msafiri atagharamia kwa hiari yake mwenyewe.

Ukatishaji tiketi mapema unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa kupitia tovuti ya festjet ambayo ni www.fastjet.com kupitia kwa mawakala wa shirika hili, ama mteja anaweza kupiga simu Namba 0784 108900. Malipo kwa ajili ya tiketi yanaweza kufanyika taslimu ama kwa kutumia benki ama kwa njia ya mitandao ya simu za mikononi.

Fastjet imepanua wigo wa ofisi zake na kwa sasa wanaendesha shughuli zao kimataifa kati ya Dar es Salaam ambako ndiyo ofisi kuu na kushirikiana na Johannesburg Afrika Kusini, Lusaka-Zambia, Entebbe - Uganda, Harare-Zimbabwe na Lilongwe nchini Malawi. fastjet pia hufanya safari zake kwenda Entebbe.

fastjet pia hufanya safari zake za ndani ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na pia kati ya Kilimanjaro na Mwanza. Safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar itaanza tarehe 11th Januari 2016.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake