Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akiwaaga watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu mpya wa Wzara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akimtambulisha kwa Watumishi wa Wizara hiyo, (hawapo pichani), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijitambulish kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo, katika mkutano wa kujitambulisha uliofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi. Meja Jenerali Rwegasira aliteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akimkabidhi Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali Projest Rwegasira, moja ya Nyaraka za Ofisi za Wizara hiyo kama ishara ya kumkabidhi ofisi.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa katika mkutano wa kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, na kuwakaribisha Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya. Hafla hii ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake