Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali tanzania anakusudia kuyachukulia hatua Mashirika
yanayoendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka
2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005.
Taarifa iliyotolewa leo na ofisi
hiyo imesema mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za
mwaka kwa kipindi cha miaka miwili pasipo kutoa sababu za msingi,
kulipa ada ya mwaka au kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa
chini ya Sheria ya NGOs.
Kwa taarifa hii, Mashirika husika
yanatakiwa yawe yamerekebisha dosari tajwa ndani ya siku thelathini
(30) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya kipindi hicho, Msajili
wa NGOs atayafutia usajili.
Mashirika ambayo yatakuwa
hayajawasilisha taarifa na kuyachukulia hatua stahiki Mashirika
yanayoendesha shughuli za NGOs bila ya usajili chini ya Sheria
husika.
Malipo yote ya ada yafanyike kupitia
Benki ya NMB, NGO Account Na. 20110014074 na stakabadhi halali ya
malipo itumwe kwa Msajili wa NGOs.
Imetolewa na:
M.S. Katemba
MSAJILI WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
06 Januari, 2015
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake