Sunday, January 24, 2016

MABONDIA ABDALLAH PAZI NA GORGER DIMOSO WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 BAGAMOYO MKOA WA PWANI

Bondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya kutia saini za makubaliano ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani 
Bondia Geoger Dimoso akisaini mkataba wa kuzipiga na Abdallah Pazi wa pili kushoto kulia ni mlatibu wa mpambano huo Pembe Ndava na kushoto ni kocha Mbaruku Heri
Mabondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani katikati ni mratibu wa mpambano uho Pembe Ndava 


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Abdallah Pazzi na Gerger Dimoso wamesaini mkataba wa kuzipiga Bagamoyo mkoa wa Pwani March 5 katika uzito wa kg 74

akizungumza wakati wa kutiliana saini Promota wa mpambano uho Muhusin Sharif amesema kuwa wameamua kupeleka mpambano uho Bagamoyo kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa pwani wapate burudani ya masumbwi siku hiyo

aliongeza kwa kusema kuwa anaomba makampuni mbalimbali kutoa sapoti kwa ajili ya udhamini wa mapambano hayo kwa kuwa Bagamoyo mchezo huo unapendwa na ndio unachipukia hivyo anaomba sapoti kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia mchezo uho ili uendelee kukua hapa nchini

ambapo kwa Bagamoyo atuna jukwaa 'ring' la ngumi ata moja mpaka tukodishe kutoka Dar es salaam yaje hapa ndio vijana wapate kucheza hivyo naomba wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia upatikanaji wa jukwaa hiro kwa ajili ya mchezo wa ngumi ili zisonge mbele

siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Sadiq Momba atakumbana na Baina Mazola katika uzito wa kg 59 na Adam Yahaya atakumbana na Selemani Bagaiza katika uzito wa kg 49 na Juma Khan atapambana na Bruno Vivuaviwili na Abdallah Zamba atakumbana na Twalibu Tuwa

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake