Thursday, January 7, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA NYAMAGANA KUKOMALIA UJENZI WA MAEGESHO JJINI MWANZA

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula (CCM, ameahidi kushughulikia suala la ujenzi wa maegesho ya magari makubwa ya mizigo nje ya jiji la Mwanza ili kuzuia magari hayo kuingia katikati ya jiji.
Akizungumza ofisini kwake hii leo, Mabula amebainisha kuwa upo mpango wa kujenga maegesho hayo katika maeneo yaliyo nje ya Jiji la Mwanza, hatua ambayo itasaidia magari hayo kutoingia katikati ya Jiji na hivyo kuondoa malalamiko yaliyopo kutoka kwa madereva wa magari madogo ya mizigo wanaolalamikia uingiaji wa magari makubwa ya mizigo katikati ya jiji.
Ameyataja maeneo yanayotarajiwa kujengwa maegesho hao kuwa ni Buhongwa pamoja na Igoma na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika, magari yote makubwa ya mizigo hayataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji.
Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi uliomalizika mwaka jana, amebainisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kufanyika kwa uharaka zaidi ambapo amewahimiza wawekezaji mbalimbali kujitokeza ili kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.

Suala la magari makubwa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza huku yakiwa na mizigo, linalalamikiwa na madereva wa magari madogo ya mizigo kwa kile wanachoeleza kuwa wanaingiliwa katika shughuli ambazo wao wangezifanya na hivyo kujiingia kipato ambapo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoruhusu magari hayo kuingia katikati ya Jiji.

Bonyeza PLAY Hapa chini Kusikiliza 

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari ofisini kwake.

1 comment:

  1. Kea ujumla serikali.inatakiwa kukaa na kuliangalia upya swala la maegesho ya magari nchi nzima. Hili ni pato kubwa sana. Linaonekana kudharauliwa na kukabidhiwa watu binafsi au makusanyo kufanywa kwa cash kiholela. Ni vyema kukawepo na mkakati maalumu na muda pia ukazingatiwa lazima kila wilaya na mkoa utakusanya mapato mazuri ya kuendeleza barabara miji na usafi. Fedha nyingi zinatagunwa nankupeleka kidogo sana. Magari yaliyopo nchini sasa hivi ni njia mojawapp ya mapato. Pia swala la ulipaji wa insurence za magari ni mdogo sana kuzingatia mlipaji analipa mara moja kwa mwaka.! Aidha ilipwe kwa kila mwezi au kwa miezi sita!! Wazo la mpita njia. Makusanyo.!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake