Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Alphonce Mchumiatumbo amesaini mkataba wa kuzipiga na Benki Mwakalebelajanuary 30 katika ukumbi wa sativa Kyela Mbeya mpambano uho wa raundi nane wa uzito wa juu utafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa uho
akisaini mkataba uho mbele ya Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa amesema ata akikisha kuwa mabondia wa uzito wa juu wanakuwa juu zaidi kwa mapambano hayo katika uzito uho
Mchumiatumbo alisema kuwa kwa sasa yupo katika mazoezi mazito chini ya kocha wake
Juma Urungu 'Mkebezi'
ambapo kwa siku amekuwa akifanya mazoezi mara mbili au tatu kwa ajili ya kujiandaa na mpambano uho
nae Rais wa TPBC Chaurembo Palasa ameongeza kwa kusema chama chao kimejizatiti kuinua mchezo wa ngumi kwa kufata taratibu na sheria za mchezo uho wa masumbwi nchini
kwanza wata akikisha kila bondia anapima afya na uzito wake kwa usalama wa mabondia wenyewe na usalama wao wawapo mchezoni
aliongeza kwa kusema kuwa watapima afya siku tano kabla ya mpambano huo ili kujilidhisha na afya za mabondia hawo wenye uzito wa juu nchini ambapo mabondia hawo wamekuwa adimu sana hapa nchini
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake