Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York, New Jersey, Connecticut na Pennsylvania unawajulisha Wanajumuiya wote kuwepo kwa mkutano na Muheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi utakaofanyika Jumamosi January 9, 2016 kuanzia saa nane kamili mchana (2:00PM) katika ofisi zetu za uwakilishi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York (Tanzania House)
Anuani: 307 E.53rd Street,New York,NY,10022.
Tafadhali zingatia muda. Uongozi unasisitiza Wanajumuiya kufika mapema ukumbini ili tupate muda wa kutosha na Muheshimiwa Balozi. Pamoja na kuja kujitambulisha kwetu Muheshimiwa Balozi atafuatana na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi. Uongozi wa NYTC pia unakumbusha wanajumuiya umuhimu wa kufanya majadiliano yote kwa amani na ustaarabu bila malumbano ya kubomoa badala ya kujenga.
Asanteni sana na karibuni.
Uongozi NYTC
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake