Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya ( hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara katika Mpaka wa Tunduma na Zambia .
Baadhi ya waandishi wa Habari Mkoani Mbeya wakiwa makini kumsikiliza Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Kishatu Kijaji katika ofisi za Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani humo kwa lengo la kutoa tathimini yake ya ziara aliyoifanya katika Mpaka wa Tunduma na Zambia.
Na
Jamiimojablogu,Mbeya
Naibu waziri
wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa
wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa ajili kudhibiti mapato
yanayopotea kutokana na kushamili kwa biashara ya ubadilishaji wa fedha
kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.
Naibu waziri
huyo ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato
(TRA) Mkoani humo na kutoa tathimini ya ziara yake aliyoifanya
katika Mpaka wa Tunduma na Zambia.
Amesema
serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara
hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo ameitaka mamlaka
hiyo kuhakikisha inaweka mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato
yake kutokana na biashara hiyo.
Amesema
serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjali na
kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa
kodi.
Amebainisha
kuwa nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi
na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu.
Sehemu
nyingine ambayo ameiagiza mamlaka hiyo kuishughulikia mara moja ili
serikali iweze kupata mapato yake ni pamoja kuibuka kwa Saccos pamoja vikundi
mbalimbali ambavyo vimekuwa vikijihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa liba kubwa
hali ambayo pia imekuwa ikiwapa mzigo mkubwa wananchi .
Katika hatua
nyingine Naibu waziri huyo ameuagiza uongozi wa mamlaka ya mapato (TRA)
Katika mpaka wa Tunduma na Zambia kuhakikisha kuwa mizigo yote inayosafilishwa
kupitia mpaka huo inafanyiwa tathimini na kulipiwa kwa muda wa usio zidi siku
moja tayari kuendelea na safari kwa inayoingia na kutoka nje ya Tanzania.
Ziara ya
Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza Mkoani Mbeya tangu alipoteuliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa
huo.
No comments:
Post a Comment