Wednesday, January 6, 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni, wakati wa mkutano wa kuzungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Johannes Msumule akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni alizungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake