Monday, January 11, 2016

Pam D azindua Video yake ya Popo Lipopo Maisha Basement

PAM D (70) PAM D (71)Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Pamela Daffa akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwenye uzinduzi wa video yake ya Popo Lipopo ndani ya Maisha Basement usiku wa kuamkia leo.

PAM D (72) PAM D (73)Pam D akifanya yake na Mesen Selekta.
PAM D (74) PAM D (75)Pam D (mwenye kipaza sauti) akichana freestyle mbele ya mashabiki wake.
PAM D (64)Madensa wa Pam D wakiendelea kufanya yao.
PAM D (69)Pam D akicheza na Madensa wake.PAM D (50)Msanii na Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, Mensen Selekta akifanya yake.
PAM D (53)
PAM D (49)...Mashabiki wakiendelea kujiachia.
PAM D (38) PAM D (59)...Wakiendelea kujiachia.
Usiku wa kuamkia leo, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa 'Pam D' kwa kushirikiana na mtayarishaji na mwanamuziki hatari Bongo, Mesen Selekta walikinukisha vya kutosha ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar.
Usiku huo uliotawaliwa na redcarpet ya hatari ambapo mashabiki kibao walipata nafasi ya kupiga picha na Pam sambamba na kuzungumza naye mawili-matatu, ulianza kwa kwa Mesen kupanda na kundi zima la Team Selekta ambapo alipopanda Mesen aliwapagawisha vilivyo na ngoma zake zote kali kama vile Kanyaboya, Sweetlove, Team Selekta pamoja na wimbo wake mpya wa Love Me.
Shangwe zilizidi pale walipopanda madensa wa PAm D kwa sarakasi kibao na madoido ambapo Pam alitokelezea na kuanza kuvurumusha nyimbo zake zote kali kuanzia Nimempata kisha akamalizia na Popo Lipopo ambapo mashabiki walipata fursa ya kuuona kwa mara nyingine live ukumbini hapo.
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake