Tuesday, January 5, 2016

Simba aua baba, mtoto

By Mussa Mwangoka, Mwananchi

Sumbawanga. Simba amevamia nyumba ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Sitalike wilayani Mlele mkoani Katavi na kuwaua watu wawili.

Taarifa zilizopatika kutoka wilayani humo jana, zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea jana alfajiri. Kijiji hicho kiko jirani na Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Stalike, Christopher Anjelo aliwataja waliouawa ni John Jeremia (45) na mwanaye wa kiume ambaye jina lake halikufahamika.

Alisema wanafamilia hao walikuwa wamelala ndani na mara Simba huyo jike alisukuma mlango ambao haukuwa imara na kuingia ndani na kuwashambulia.

Alisema mke wa marehemu alifanikiwa kukimbia.

Hata hivyo, alisema baada ya taarifa kusambaa, wanakijiji waliamua kumsaka na kumkuta akiwa amejificha kichakani na pembeni kukiwa na kichwa cha mtoto huyo aliyeuawa.

Alisema simba huyo aliuawa na askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Katavi.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake