Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongea na Waandishi wa habari kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.
13/01/2016
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha Mapinduzi kila mwaka huadhimisha
kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Februari 05, 1977. Mwaka huu kitakuwa kinatimiza miaka 39.
- UZINDUZI
Uzinduzi
wa maadhimisho ya kumbukumbu ya hiyo utafanyika tarehe 31 Januari, 2016 Unguja,
Zanzibar ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa
Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein.
- KILELE CHA SHEREHE
Kilele
cha maadhimisho hayo Februari 06, 2016 mjini Singida ambapo Mgeni rasmi atakuwa
Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dokta Jakaya
Mrisho Kikwete.
Viongozi
wa kitaifa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu watakaohudhuria watapangiwa
shughuli za ujenzi wa Chama na Taifa kwa ujumla katika wilaya zote za mkoa wa
Singida siku tatu kabla ya kilele cha maadhimisho hayo.
Mikoa
yote iandae shughuli mahsusi kwa wiki nzima ya maadhimisho hayo, mkazo ukiwa ni
kufanya shughuli za ujenzi wa Chama na Taifa katika maeneo yao, Mambo ya
kuzingatia katika wiki hiyo ni kama ifuatavyo:-
i.
Kuingiza wanachama wapya wa CCM na Jumuiya
zake na kufanya shughuli nyingine za kuimarisha Chama.
ii.
Kufanya mikutano ya kuwashukuru wana CCM na
wananchi kwa kuiamini CCM kuendelea kuongoza Nchi yetu kwa kushiriki na
kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo CCM ilipata ushindi wa kishindo wa
Rais, Wabunge na Madiwani.
iii.
Kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili
kujiletea maendeleo yao binafsi na ya Taifa.
iv.
Kushiriki shughuli za maendeleo mbalimbali
ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, vituo vya afya, upandaji miti, uchimbaji
wa mitaro ya maji, kufanya usafi wa mazingira pamoja na shughuli nyingine za
kijamii.
- KAULIMBIU
Kaulimbiu
ya sherehe hizo ni “Sasa Kazi, Kujenga
Nchi na Kukijenga Chama”.
Nape
Moses Nnauye (Mb.),
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
No comments:
Post a Comment