Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kwenye Manispaa za Ilala, Temeke na Kindondoni, umebaini msongamano huo wa wanafunzi upo zaidi kwenye madarasa ya awali na la kwanza ambayo ndiyo huandiksha wanafunzi wapya.
Wingi huo wa wanafunzi umesababishwa na hatua ya baadhi ya wazazi kuwaandikisha watoto wenye umri wa miaka tisa hadi 10 ambao kwa kawaida walipaswa shule miaka mitatu iliyopita.
Wakizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini, walimu kadhaa walisema mpango wa elimu bure umewaletea changamoto nyingi ambazo kwao ni vigumu kutatua.
Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Mbagala Kizuiani alisema katika darasa moja la awali ambalo lina uwezo wa kuchukua watoto 100, mwaka huu lina wanafunzi zaidi ya 400 hali inayowawia vigumu kuwafundisha.
“Hatuwezi kudhibiti wingi wa wanafunzi kwa sasa, darasa la awali na lile la kwanza yamezidiwa na wingi wa wanafunzi," alisema mwalimu huyo na kueleza, "tunachokifanya ni kusubiri serikali kama itaangalia namna ya kufanya ili wasome vizuri.
"Kwa mrundikano kama huu, sidhani kama kuna elimu hapa.”
Uchunguzi wa Nipashe umebainisha shule zenye msongamano mkubwa wa wanafunzi katika madarasa ya awali na la kwanza ni Mbagala Kuu, Mbagala, Kiwalani, Kinyerezi, Charambe, Makangarawe, Mwenge na Reginald Mengi.
WATOTO BILA MAFAFTARI
Walimu hao walilalamikia hatua ya wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni bila vifaa kama madaftari na kalamu, wakidhani vitanunuliwa na serikali.
Akielezea hali hiyo, mwalimu wa Shule ya Msingi Kinyerezi ambaye naye hakutaka jina lake litajwe alisema wanatumia muda mwingi kuwaelimisha wazazi ambao wanaamini vifaa hivyo vipo katika mpango wa elimu bure.
“Baadhi ya watoto wamekuja bila madaftari na peni, tunapowahoji vifaa hivyo viko wapi wanatujibu kwamba wazazi wao wamewaambia watapata shuleni," alisema.
"Tunafanya kazi kubwa kuwaita wazazi na kuwaelimisha.”
Serikali imeanza kutekeleza mpango wa elimu bure kama ilivyoahidiwa na Rais John Magufuli katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, kwa kusambaza mgao wa fedha kwenye shule za msingi na sekondari kwa mwezi Januari.
Hata hivyo, baadhi ya shule hizo zilijikuta zikipewa Sh. 29,000 kama mgao wake wa mwezi, jambo ambalo limelalamikiwa na wadau wa elimu kwamba hazitoshelezi kumudu mahitaji ya wanafunzi.
Fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa nyenzo za kufundishia na kujifunzia, ukarabari wa majengo na miundombinu, uandaaji wa mitihani, michezo na matumizi ya utawala.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Vifaa hivyo lazima vipatikane shuleni. Walau sasa wazazi wamewaleta watoto wao shuleni. Serikali itawjibika kuwa na madara yenye watoto 20 per class na mwalimu. Especialy in first grade and second grade. Chekechea inapaswa kuwa na watoto 10 per class and a teacher. Jamani elimu ni mhimu sana.
ReplyDeleteSijaona mahali wakizungumzia mshahara wa walimu kupandishwa...kama mtoto atamaliza la saba bila kujua kusoma sitashangaa.
ReplyDeleteSerikali iongeze mishahara ya walimu kwanza.elimu bure + low salaries= division 0
It makes me cry to look at the picture. And our leaders wanatafuna nchi as if there is no tomorrow. JPM please - lock them at Ukonga for life.
ReplyDeleteHow on earth, nchi imeachwa hivi, previous uongozi didn't care at all.
Inaonyesha jinsi gani watoto wengi walikuwa hawasomi kwa kukosa ada. Mabillioni ya safari tulikuwa nazo lakini za kuwasomesha watoto hakuna. Mungu yupo
ReplyDelete